Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Membe: Tumepoteza mshauri masuala ya uchaguzi
Habari za Siasa

Membe: Tumepoteza mshauri masuala ya uchaguzi

Spread the love

BERNARD Kamilius Membe, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Tanzania amesema, kifo cha Rais mstaafu, Benjamin William Mkapa ni pigo kubwa kwa Taifa kutokana na umuhimu wake hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu. Anaripoti Faki Sosi, Lindi … (endelea).

Mkapa amefikwa na mauti usiku wa kuamkia leo Ijumaa tarehe 24 Julai 2020 katika moja ya Hospitali jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

         Soma zaidi:-

Mwili wake, utaagwa kwa siku tatu katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kuanzia Jumapili ya tarehe 26 hadi 28 Julai 2020 na maziko yatafanyika kijijini kwake Lupaso, Masasi Mkoa wa Mtwara Jumatano tarehe 29 Julai 2020.

Viongozi mbalimbali, wamemzungumzia Mkapa aliyezaliwa tarehe 12 Novemba 1938 na kufanikiwa kuwa Rais wa awamu ya tatu kati ya mwaka 1995-2005 kwa jinsi walivyomfahamu.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Membe ambaye ni mtia nia wa urais wa Tanzania kupitia chama cha ACT-Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020 amesema, Mzee Mkapa alikuwa miongoni mwa marais wazuri aliyetumia muda wake kusaidia jamii.

“Mzee Mkapa tutamkumbuka kwa kuwa kiongozi ambaye  alitumia muda wake mwingi kuisaidia jamii ya Tanzania, alikuwa miongoni mwa marais wazuri, kifo chake kimetuachia majonzi,” amesema Membe.

Amesema, kifo cha Mzee Mkapa kimewafanya viongozi wa ACT-Wazalendo kuahirisha mkutano mkubwa wa chama hicho ulipangwa kufanywa kesho Jumamosi Lindi mjini.

“Nazungumzia kutoka Lindi ambapo wanachama wa ACT-Wazalendo walikuwa wakutane  kesho lakini kwa sababu ya msiba huu mkubwa  ambao umetupata viongozi wa chama na sisi wenyewe tumelazimika kuahilisha shughuli hizi ili kumpa heshima mstaafu baba yetu Benjamini Mkapa na wote tutakwenda Dar es Salaam na Masasi  kushiriki kutoa rambirambi na heshima zetu,” amesema.

Membe amesema, Rais Mstaafu Mkapa alikuwa ndiye mshauri mkuu wa masuala ya uchaguzi nchini kipindi cha uchaguzi.

“Katika kipindi cha uchaguzi kama hiki alikuwa mshauri, tumepoteza mtu ambaye alikuwa akisawazisha masuala ya kiuchaguzi, alikuwa mshauri mkubwa katika masuala ya uchaguzi,” amesema Membe

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!