Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Jeshi la Polisi kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama kwa watalii nchini
Habari Mchanganyiko

Jeshi la Polisi kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama kwa watalii nchini

Spread the love

 

JESHI la Polisi limesema kuwa litaendelea kuunga mkono juhudi za Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi la ulinzi na usalama Daktari Samia Suluhu hassan Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kukuza utalii na kuongeza watalii Nchini kwa kuimarisha ulinzi na usalama kwa watalii wa ndani na nje ya Nchi. Anaripoti Abel Paul wa Jeshi la Polisi, Dar es Salaam … (endelea).  

Hayo ameyasema Mkuu wa kituo cha utafiti cha Jeshi la Polisi kilichopo chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) kamishna msaidizi wa Polisi ACP Ralf Meela katika mafunzo yaliyotolewa na wakufunzi kutoka chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kwa wanafunzi wanaoendelea na kozi mbalimbali chuoni hapo.

Amebainisha kuwa Mafunzo hayo yanakwenda kuuongeza weledi katika kutoa huduma bora kwa wageni ambao wanafika nchini kwa ajili ya utalii.

Ameongeza kuwa katika kuunga mkono juhudi hizo Jeshi la Polisi nchini limeanzisha kitengo maalum kwa ajili ya kutoa huduma za kitalii na kituo cha Polisi Utalii na Diplomasia kilichopo jijini Arusha ambacho kinahusika moja kwa moja na kutoa huduma kwa watalii na wanadiplomasia wanapokuwa Nchini.

Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Ralf Meela

Kwa upande wake Mkufunzi kutoka Chuo cha Taifa cha utalii Amiri Abdu amesema kuwa wametoa mafunzo hayo kwa Jeshi la Polisi ambao ndio wadau wakubwa katika maswala ya ulinzi na usalama na amebainisha kuwa Jeshi hilo linanafasi kubwa ya kuongeza idadi ya utali kutokana na kuimarisha ulinzi kwa watalii.

Naye Mwanafunzi wa kozi ya mkaguzi msaidizi wa Polisi Naomi Laizer amebainisha kuwa, wamejifunza na kuelewa vyema dhana ya utalii na mtalii ambapo amesema, mafunzo hayo yamekuja wakati sahihi wakati taifa linapokea wageni wengi kwa sasa na wameahidi kutoa huduma bora kwa watalii.

Malius Nyenza mwanafunzi wa kozi ya uofisa amebainisha kuwa mafunzo hayo yamewajenga na kuwaongezea maarifa katika sekta hiyo ya utalii ambayo inachangia pato kubwa katika taifa na amesema kuwa, kama Jeshi la Polisi wataendelea na utaratibu wao wa kila siku wa kuimarisha ulinzi wa raia na mali zao wakiwemo watalii wanaoingia Nchini kwa ajili ya utalii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atangaza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba

Spread the loveSERIKALI imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu ya...

error: Content is protected !!