Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Jaji Mkuu ataja mikakati kukabili uhaba wa majengo ya mahakama
Habari Mchanganyiko

Jaji Mkuu ataja mikakati kukabili uhaba wa majengo ya mahakama

Spread the love

 

JAJI Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, imepanga kujenga majengo ya mahakama katika mikoa yote yenye uhaba, ambapo ujenzi huo utaanza 2023 na kukamilika 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Prof. Juma ametoa taarifa hiyo leo Ijumaa, tarehe 25 Novemba 2022, akizundua majengo ya mahakama za wilaya 18, mkoani Simiyu.

“Baada ya kupata majengo haya (18), changamoto ya upungufu wa majengo imepunguzwa sana lakini tunaendelea kukubali kwamba maeneo mengi ya nchi yetu bado yanasubiri majengo, Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (WB), ina mpango wa kuhakikisha mikoa ambayo haina majengo ya mahakama kuu, yataanza kujengwa mwaka ujao,mikoa hiyo ya Manyara, Lindi, Singida, Geita, Songwe, Simiyu, Njombe, Katavi zote zitapa majengo ifikapo 2024,” amesema Prof. Juma.

Katika hatua nyingine, Prof. Juma amesema Serikali ina mpango wa kujenga mahakama za mwanzo katika kila tarafa, ili kusogeza huduma za kisheria karibu na wananchi.

“Nashukuru Serikali ya Rais Samia ambayo imekubali kwamba program ya maboresho ni mkakati wa maendeleo ya nchi na amekuwa akitumia neno kufungua nchi, sisi mahakama tunatafsiri kufungua nchi ni kuwa na majengo yenye huduma ambazo zinasaidia wananchi.Mahitaji ya majengo ni makubwa sana na mahakama imejiwekea vigezo cha kwanza kila wilaya inayoanzishwa lazima iwe na ngazi ya mahakama za wilaya, kila tarafa iwe na mahakama ya mwanzo,” amesema Prof. Juma.

Sambamba na hilo, Prof. Juma amesema ujenzi wa majengo ya mahakama umekuja sambamba na maboresho ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ili kuwezesha huduma zake kupatikana katika mifumo hiyo.

“Majengo yamekuja na maboresho ya TEHAMA na huduma ya mahakama sio utoaji haki, ni huduma za kupata taarifa muhimu kuhusu sheria na taratibu za Tanzania, hizi zote zinapatikana katika mifumo ya TEHAMA ambazo itaanzia hapa, ndio maana tunasema tunaelekea mifumo ya teknolojia huduma hazitategemea majengo, zitapatikana kwa mfumo wa TEHAMA ambao uatsaidia kusogea haki karibu na wananchi,” amesema Prof. Juma.

Prof. Juma amesema, tathimini iliyofanywa na Mahakama ya Tanzania 2015, ilionyesha wilaya 104 kati ya 139 za Bara, zinahitaji majengo mapya na kwamba majengo 18 yaliyozinduliwa leo yatapunguza uhaba huo.

Awali akitoa taarifa fupi ya mradi wa ujenzi wa mahakama hizo 18, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Profesa Elisante Ole Gabriel, amesema umegharimu Sh. 18.3 bilioni, ambapo kila mahakama imegharimu Sh. 1 bilioni ikiwemo gharama za samani.

Prof. Elisante ametaja baadhi ya mahakama hizo, ikiwemo Mahakama ya Wilaya ya Busega, Gairo, Kilombero, Mvomero, Kakonko, Uvinza, Kaliuwa na Misenyi.

“Mradi huu wa utekelezaji wa mpango mkakati wa mahakama wa 2021 hadi 2025, lakini pamoja na mpango wa ujenzi wa 2022 hadi 2026. Utekelezaji wa mradi huu umetumia mkopo wa Benki ya Dunia, ulichukuliwa mkopo wa bei nafuu na kuwezesha mradi kufanyika,” amesema Prof. Elisante.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!