May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Haji Manara aibukia Yanga, atambulishwa rasmi

Spread the love

 

ALIYEKUWA msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara ametambulishwa rasmi ndani ya klabu ya Yanga, mara baada ya kuachana na wajiri wake wa zamani. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Manara ametambulishwa na uongozi wa Yanga, hii leo Agosti 24, 2021 jijini Dar es Salaam kwenye hotel ya Serena jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari na kukabidhiwa rasmi jezi ya klabu hiyo.

Wakati akimtambulisha msemaji huyo, mshauri Mkuu wa klabu ya Yanga, Senzo Mazingisa alisema kuwa wameamua kumrudisha Haji Nyumbani kwa kuwa ndipo alipotoka.

“Napenda kuchukua nafasi usiku huu kumtambulisha mtoto wa nyumbani ambaye amerejea kwao kwenye klabu ya Yanga”Alisema Senzo

Haji ambaye alidumu kwenye klabu ya Simba kwa miaka Sita na kuamua kuachana na klabu hiyo, mara baada ya kuingia katika mgogoro mzito na mtendaji mkuu wa klabu Simba Barbara Gonzalez mwezi Julai.

Mara baada ya kupewa nafasi ya kuongea mbele ya waandishi wa Habari, msemaji huyo wazamani wa klabu ya Simba alinena kuwa atafanya kazi mara 10, Zaidi aliyoifanya akiwa na Simba katika kipindi cha miaka sita.

“Niwahakikishie wana Yanga, nitafanya kazi mara 10 zaidi ya niliyoifanya ndani ya Simba na najisikia raha kufanya kazi na klabu kubwa Afrika Mashariki na msimu huu tutachukua kombe bila manung’uniko yoyote” Alinena Haji

Katika hatua nyingine klabu hiyo itazindua jezi zake kesho Agosti 25, kuelekea msimu mpya wa mashindano kwenye ukumbi wa Mlimani City.

error: Content is protected !!