
Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC)
MUUNDO wa sasa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), uko mbioni kufanyiwa marekebisho makubwa ya kisheria, baada ya kuibuka malalamiko kutoka kwa wadau wa uchaguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa za ndani ya Tume hiyo, zinaeleza kuwa pamoja na mambo mengine, muundo mpya wa NEC unalenga kuwaondoa wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, manispaa na majiji, kuwa wasimamizi wa uchaguzi.
Kuondolewa kwa wakurugenzi hao kuwa wasimamizi wa uchaguzi, kunatokana na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wadau wa uchaguzi, hususani vyama vya upinzani, kuwatuhumu kupendelea wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Malalamiko hayo yalipata nguvu zaidi katika uchaguzi mkuu uliopita, baada ya maeneo kadhaa ambayo ni ngome ya upinzani kuchukuliwa na CCM katika kile vyama hivyo vinakiita, “uporaji wa uchaguzi.”
Undani wa habari ikiwemo kujua mapendekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Soma Gazeti la Raia Mwema toleo la leo Jumatano, tarehe 25 Agosti 2021.
More Stories
#LIVE: Tuzo za EJAT2021, Majaliwa atoa ujumbe kwa MCT
Ni Profesa Hoseah tena TLS
Askofu Gwajima: Viongozi wa Serikali wanamchonganisha Rais