Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa DP yaja na ‘Mlete Mzalendo Twende Pamoja’
Habari za Siasa

DP yaja na ‘Mlete Mzalendo Twende Pamoja’

Spread the love

CHAMA cha Democratic (DP) kimekuja na ‘Kampeni ya Mlete Mzalendo Twende Pamoja’ yenye lengo la kujenga chama na kuhakikisha kinafanya vizuri katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na uchaguzi mkuu wa 2025. Anaripoti Suleimani Msuya, Dar es Salaam … (endelea).

Kampeni hiyo imezinduliwa leo tarehe 29 Oktoba, 2022 jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa chama hicho Abdul Mluya katika ofisi za makao zilizopo Mburahati wilayani Ubungo.

Mluya amesema kampeni hiyo ilizinduliwa rasmi mkoani Dodoma Oktoba 5,2022, ila baada ya kuzinduliwa hapa mkoani Dar es Salaam itaanza kufanyika katika mikoa yote ya Tanzania hadi kufikia wakati wa uchaguzi.

Katibu Mkuu wa DP, Abdul Mluya akimkabidhi kadi mwanachama mpya wa chama hicho, Grace Massawe, baada ya uzinduzi wa ‘Kampeni ya Mlete Mzalendo Twende Pamoja’ iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu huyo amesema wakati wanaendelea na kampeni hiyo, watakuwa wanaandaa wanachama wao kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vijiji, vitongoji, udiwani na ubunge.

“Oktoba 5, 2022 kwenye makao makuu madogo ya chama jijini Dodoma tulizindua kampeni ya ‘Mlete Mzalendo Twende Pamoja’ na leo hii tumezindua hapa jijini Dar es Salaam, ambapo tumeanza kukusanya wanachama wetu mmoja mmoja, nyumba kwa nyumba na mtaa kwa mtaa bila kuvunja sheria.

Lakini pia tutatumia kampeni hii kuwaanda wagombea wetu kuanzia ngazi ya kitongoji, kijiji, mtaa, udiwani na ubunge,” amesema.

Amesema wanaamini kuwa watanzania wenye uzalendo wataungana nao katika kampeni hiyo ambayo inaenda kulikomboa taifa kifkra na maendeleo.

Mluya amesema kwa sasa wataenda mikoa mitano ya Tanzania Bara na baadae wataenda Unguja na Pemba na kurejea upande wa bara katika wilaya na mikoa iliyobakia.

Amesema kampeni hiyo itajikita katika kuwapatia wananchi elimu ya uraia, ili waweze kujua thamani ya kura na kuondokana na kundi kubwa la wananchi wanajiandikisha kutopiga kura.

“DP tumefanya tathmini ya kina na kutambua kuwa sisi ndio baba wa vyama vya siasa hasa vya upinzani, tunataka watu wakijiandikisha milioni 21 wajitokeze kupiga kura, kwani huu utaratibu wa idadi ndogo kushiriki kupiga kura haikubaliki,” amesema.

Katibu Mkuu huyo amesema kupitia elimu ya uraia ambayo wanaendea kutoa wanaamini wataenda kushinda katika chaguzi zote, huku washindani wao wakiwa na nyuso za furaha kwani watashindwa kwa haki.

Amesema uzinduzi huo utazingatia katazo la mikutano ya hadhara, hivyo watatumia njia ya mikutano ya ndani ambayo imeruhusiwa, ili dhamira yao ya uzalendo iweze kutawala katika kila hatua.

Aidha, Mluya ametoa raia kwa Rais Samia Suluhu Hassana, kufanyia kazi mapenfekezo ya ripoti ya Kikosi Kazi, ili kuhakikisha malalamiko wakati wa uchaguzi yanafikia mwisho na mwenye haki aweze kushinda kihalali.

“Tunataka kuona utekelezaji wa ripoti ya Kikosi Kazi ukianza mapema ili dhana ya kuwa na chaguzi za kidemokrasia inatawala,” amesema.

Amesema iwapo mapendekezo yaliyotolewa na Kikosi Kazi yatapewa kipaumbele ni wazi kuwa changamoto zilizotokea uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2019 na uchaguzi mkuu wa 2020 hataweza kutokea.

Mluya amesema DP haitavumili uvunjifu na uonevu wowote ambao utatokea katika mchakato wa chaguzi hizo zijazo kwa kuwa watakuwa wametengeza wafuasi wao wanaojitambua kupitia utoaji wa elimu chini ya kampeni ya Mlete Mzalendo Twende Pamoja.

Katibu huyo amewataka viongozi na waratibu wa chama hicho kufanya kazi ya kunjenga chama kwa kufuata Katiba na sheria za nchi, hivyo kulitaka Jeshi la Polisi kutokuwa kikwazi kwa kampeni hiyo.

“Tunaenda kufufua DP upya, haturudi nyuma na sitaki kusikia Jeshi la Polisi likishiriki kukwamisha mipango yetu, hatutakubali,” amesema.

Amesema katika kuonesha nia yao ya kufufua chama wameanza kupokea wanachama wapya katika mikoa mbalimbali nchini.

Pia, Mluya amemtaka Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kujitafakari katika nafasi hiyo, kutokana na adha ya maji ambayo wananchi wa Dar es Salaam wanapitia.

Amesema waziri huyo anapaswa kuchukua hatua ya kuachia ngazi ili kumpatia nafasi Rais Samia kumpa mtu mwingine aweze kuwavusha.

“Hii ni aibu katika taifa lenye miaka 60 ya uhuru bado wananchi wake wanateseka kwa shida ya maji, hii haikubali naomba Rais Samia ampangie kazi nyingine Wzairi Aweso kwani ameshindwa na niabu kwa jiji la kibiashara kukosa maji,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!