Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Tulia: Mchango wa NMB umechochea maendeleo Tz, Z’bar
Habari Mchanganyiko

Dk. Tulia: Mchango wa NMB umechochea maendeleo Tz, Z’bar

Spread the love

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (BJMT), Dk. Tulia Ackson na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), Zubeir Ali Maulid, wamekiri kuwa mchango wa Benki ya NMB kwa maendeleo ya Taifa unaakisi ukubwa na uimara wa taasisi hiyo, huku wakiitaka kudumisha ushirikiano na mihimili hiyo ya dola, pamoja na Serikali za pande zote za Muungano. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Dk. Tulia ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Maulid, wametoa kauli hizo wakati wa hafla ya Usiku wa Tuzo kwa washindi na mabingwa wa bonanza lililoshirikisha timu za wafanyakazi wa NMB na wabunge wa BJMT na BLW, lililofanyika tarehe 11 Januari 2024 ikiwa ni sehemu ya Sherehe za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akitoa neno la shukrani kwa kudhamini bonanza hilo, Dk. Tulia aliipongeza NMB kwa namna inavyotumia vema fungu la Programu ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), ambako imezisapoti pakubwa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan na ile ya Dk. Hussein Ali Mwinyi, kupambana na changamoto zinazokwaza ustawi wa sekta za elimu, afya, majanga na mazingira.

“Nitumie fursa hii kuwashukuru sana NMB, kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha kwa Baraza la Wawakilishi kufanikisha bonanza hili, ambalo limegharimu kiasi kikubwa cha pesa, lakini mkashirikiana kufanya liwe zuri. Na mashirikiano yenu yapo kwa Serikali zote yaani ya Tanzania na ile ya Zanzibar katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

“Hapa tumesikia kitu kisicho cha kawaida, Mbunge kutoka chama kisicho cha Mapinduzi, akisifia kazi nzuri inayofanywa na Dk. Mwinyi na Dk. Samia, maana yake ni kuwa kazi za marais hawa wawili zimepitiliza, hata usipotaka kuziona utaziona tu. Sasa NMB ni sehemu ya kazi hizo na ndio maana naipongeza sana sana kwa ushirikiano mzuri ambao mnautoa kwa Serikali zetu.

“Na kwa kweli sisi kama Wabunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, tunauona mchango wenu, tunasikia huku mmetoa madawati, kule vifaa vya kuezekea yakiwemo mabati, vifaa tiba, ujenzi wa madarasa na kadhalika, kutokana na asilimia moja ya faida yenu mnayotenga kurejesha kwa jamii.

“Na kimsingi mko vizuri hata katika yale mambo makubwa makubwa yale, hesabu zenu kama benki ziko juu, namba zenu ni nzuri, sifa zimuendee CEO wenu  Ruth Zaipuna anafanya nzuri sana,” alibainisha Dk. Tulia akiitaka NMB kufikiria namna ya kushiriki ujenzi wa viwanja ili kutanua wigo wa wananchi kuunga mkono jitihada za Dk. Mwinyi na Dk. Samia kuhimiza kufanya mazoezi.

 Akimkaribisha Spika Tulia kuzungumza, Spika wa BLW, Zubeir Ali Maulid, alisisitiza umuhimu wa NMB kudumisha ushirikiano na Serikali za pande zote mbili za Muungano, pamoja na mabunge, kwani kufanya hivyo ni moja ya kudumisha na kustawisha Muungano ulioasisiwa na waanzilishi wake marais wa kwanza wa Tanzania Bara na Zanzibar.

 Awali, Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Juma Kimori, alilishukuru Baraza la Wawakilishi, Spika na Wajumbe wake kwa kuichagua NMB kushirikiana nayo katika kufanikisha bonanza hilo na kusisitiza kwamba taasisi yake ikiwa ni mdau namba moja wa Serikali zote mbili, itaendeleza mashirikiano makubwa yaliyopo, kwani wanajali na kuthamini ushirikiano huo.

“Binafsi niseme nimefarijika sana kwa aina ya ushirikiano uliopo baina ya Bunge la Tanzania na Baraza la Wawawkilishi, nasi tumefanya makubwa kila upnade, hata hapa Zanzibar tumefanya mashirikiano makubwa na uthibitisho ni juzi tu NMB ilitoa mikopp ya boti ili kuendeleza adhma ya Serikali ya kukuza uchumi wa bluu.

“Kama benki ambayo ipo kila sehemu nchi nzima na hapa tupo mbele ya wawakilishi wa wananchi, mtakuwa mashuhuda kuwa kila mbunge na mwakilishi hapa, NMB imegusa maisha ya wananchi wake, iwe kwenye elimu, afya, ujasiriamali, na hata majuzi tumezindua mikopo ya MastaBoti kule Pemba, lengo ni kugusa na kuboresha maisha ya Watanzania.

“Kwa hiyo tunaahidi tutaendelea kushirikia na nyie, kupitia asilimia moja ya faida yetu. Tunawakaribisha wabunge na wawakilishi wote kuja NMB wanapohisi kuna changamoto majimboni ambazo tunaweza kujadiliana na kuona namna ya kuzitatua,” alisema Kimori aliyemwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wake Ruth Zaipuna, ambaye alibanwa na majukumu mengine.  

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara yaomba bajeti ya Sh. 67.9 bilioni, wamachinga watengewa bilioni 10

Spread the loveBAJETI ya Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Migogoro ya ndoa yaongezeka, Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveMIGOGORO ya ndoa na familia imeongezeka kwa asilimia 8.3  kutoka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yahamasisha uanzishaji vituo vya kulea watoto wachanga

Spread the loveSERIKALI imewahimiza wananchi kujenga vituo vya kulelea watoto wadogo na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

error: Content is protected !!