Saturday , 18 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Shoo kuzikwa Jumatano Dar
Habari Mchanganyiko

Dk. Shoo kuzikwa Jumatano Dar

Dk. Gideon Juma Safari Shoo
Spread the love

 

MWANDISHI wa habari mkongwe nchini, Dk. Gideon Juma Safari Shoo, aliyefariki dunia tarehe 9 Julai, 2022, akiwa na umri wa miaka 66, atazikwa Jumatano mchana, tarehe 13 Julai, mwaka huu mjini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Msemaji wa familia ya Shoo, Bwana Kodi Siarra, amethibitisha jana tarehe 10 Julai kuwa Dk. Shoo atazikwa katika Makaburi ya Kondo, Kunduch, Dar es Salaam, mchana wa Jumatano.

Mazishi ya Dk. Shoo yatatanguliwa na ibada ya kumuaga mwandishi wa habari huyo msomi na nguli, itakayofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Dk. Shoo ni mwanzilishi na mwanahisa wa Shule hiyo.

Shughuli hiyo ya kumuaga Dk. Shoo itaanza saa tano asubuhi kufuatia siku nne za msiba unaoendelea nyumbani kwake, Salasala, mkabala na mitambo ya umeme ya IPTL.

Dk. Shoo aliaga dunia baada ya kupigania maisha yake kwa siku 16 katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali ya Muhimbili Orthopaedic Institute (MIO) iliyopo Hospitali Kuu ya Taifa ya Muhimbili, Dar Es Salaam.

Dk. Shoo alifikishwa Moi asubuhi ya Alhamisi tarehe 23 Juni, mwaka huu baada ya kupata shambulio kubwa la kiharusi cha kichwani (hemorrhage stroke) kilichopasua baadhi ya mishipa ya damu, na alipoteza fahamu akiwa njiani kupelekwa Muhimbili.

1 Comment

  • Acha lifariki hata kama nami siku moja nitafuata. Lilikuwa noko na lenye roho mbaya pamoja na salva rweyemamu na said kubenea. Naona yanateketea mmoja baada ya mwingie. Amina

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RUWASA yachongewa, yateketeza mamilioni kwa maji yenye magadi

Spread the loveSAKATA la ukosefu wa maji wilayani Momba mkoani Songwe limezidi...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua bima ya afya kwa wakulima

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni...

error: Content is protected !!