Sunday , 23 June 2024
Home Habari Mchanganyiko DAWASA yaja na suluhisho la maji kwa wakazi wa Sinza C,D
Habari Mchanganyiko

DAWASA yaja na suluhisho la maji kwa wakazi wa Sinza C,D

Spread the love

Wakazi wa Kata ya Sinza, Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam wametolewa hofu ya upatikanaji wa huduma ya maji kwenye maeneo yao kutokana na jitihada kubwa zinazotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) za kufikisha huduma ya maji kwa uhakika. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Diwani Kata ya Sinza, Raphaeli Awino ameeleza hayo alipotembelea mradi wa kuongeza huduma ya maji ambao umeanza kutekelezwa na mamlaka hiyo kwa lengo la kuondoa changamoto ya uhaba wa maji Sinza.


Amesema kuwa eneo la Sinza hususani mtaa wa Sinza C na D limekuwa kwenye changamoto ya upatikanaji mdogo wa maji kwa muda sasa kutokana na maji kuwa na msukumo mdogo, lakini kutokana na jitihada zinazoendelea kutekelezwa na DAWASA, ikiwemo za mradi wa kuongeza maji Sinza C na D, hali hiyo itaenda kuisha karibuni.

“Leo nimetembelea na kuona kazi kubwa inayofanywa na DAWASA, naishukuru Serikali yetu na nimpongeze na kumshukuru sana Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa utayari wake wa kuelekeza fedha nyingi kwenye miradi ya huduma ya majisafi kwa wananchi wake, hii ishara ya upendo kwa watanzania wote,” ameeleza Raphaeli.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi huu Meneja wa Mkoa wa kihuduma DAWASA Magomeni, Julieth John amesema kuwa mradi huu unatekelezwa kwa lengo la kuongeza msukumo wa maji kwenye eneo la Sinza C na D ambalo linapata maji wa msukumo mdogo.

“Hivyo kutokana na hali hiyo, kazi kubwa imeanza kufanyika inayohusisha uchimbaji na ulazaji wa mabomba ya inchi 6 kwenye eneo la umbali wa kilomita 1 na mita 30, kuanzia eneo la ubungo maji hadi njia panda ya kuingia Mawasiliano, ambapo litaungwa kwenye mtandao mwingine wa bomba la inchi 6 kwa lengo la kuongeza msukumo wa maji kwenye eneo la Sinza,” amesema.

Ameongeza kuwa kwa sasa wanaongeza upatikanaji wa maji kutoka kwenye Mtambo wa Ruvu Juu ili kuongezea kiasi cha maji kinachotoka kwenye Mtambo wa Ruvu chini.

“Kazi hii inatarajiwa kukamilika mapema mwezi huu na kuwezesha wananchi wote wa Sinza kufurahia huduma, hivyo niwape Imani ya kupata maji kwa wingi katika kipindi kifupi,” ameeleza Julieth.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Askofu Wolfang Rais mpya TEC, Padri Kitima aula tena

Spread the loveBARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetambulisha safu mpya za...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washiriki mbio za NBC Dodoma Marathon kutumia treni ya SGR kwenda Dodoma

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

Habari MchanganyikoTangulizi

Padre anayetuhumiwa mauaji ya Asimwe, asimamishwa

Spread the loveKanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji...

Habari Mchanganyiko

Upandaji miti uzingatie kuondoa umaskini kwa wananchi

Spread the loveKATIBU Tawala wa mkoa wa Morogoro Dk. Musa Ally Musa...

error: Content is protected !!