Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Chavita waomba elimu kwa viziwi, barakoa tatizo kwao
Habari Mchanganyiko

Chavita waomba elimu kwa viziwi, barakoa tatizo kwao

Spread the love

CHAMA cha Viziwi Mkoa wa Dodoma (CHAVITA) kimeiomba serikali kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoa elimu kwa jamii ya Viziwi juu ya kujikinga na maambukizi yanayosababishwa na virusi vya Corona. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Dodoma, Amina Issah, alisema kuwa viziwi wapo hatarini kupata maambukizi ya virusi vya Corona kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya kujikinga na ugonjwa huo.

Alisema kuwa vyombo vingi vya habari pamoja na sehemu mbalimbali hakuna wakalimani wa kutosha jambo ambalo linasababisha jamii hiyo kutokuwa na uelewa wa jinsi ya kujikinga na maambukizi hayo.

Amina ambaye naye ni Kiziwi alisema kuwa kuna haja kubwa ya serikali kuongeza walakimani katika maeneo mbalimbali muhimu kama vile hospitali, vituo vya polisi, makanisani na misikitini ili nao waweze kuelewa na kujikinga na maambukizi hayo.

“Kuna changamoto kubwa kwa  watu wenye ulemavu wa kutokusikia kutokana na kuwa  na uelewa mdogo na wanahitaji kuambiwa na kuelimishwa ana kwa ana kwa asilimia kubwa wengi hawana elimu hasa waliopo pembezoni na hasa serikali imewasahau hasa wanapotia matangazo na taarifa mbalimbali wakati hakuna wakalimani.

“Kukosekana kwa wakalimani kunasababisha kuchelewa kupata taarifa na kujikuta hawajui namna bora ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona na kutoelewa ni wapi watakwenda iwapo watapata maambukizi ya ugonjwa huo,” alieleza Amina.

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa chama hicho kinaishauri serikali iwakumbuke viziwi kwa kuwawekea wakalimani wa kutosha katika kipindi chote ambacho wanatoa matangazo yanayohusu matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu jinsi ya kujilinda na maambukizi ya virusi vya Corona.

“Itapendeza zaidi serikali kupitia Wizara husika kuandaa vipindi vilivyotafusiriwa kwa lugha ya alama na kuvirusha katika luninga ikiwa ni sehemu ya kutoa elimu kwa jamii ya watu ambao ni viziwi, pia ni vyema kuangalia ni namna gani ya kuweza kufikisha ujumbe kwa walemavu hao hasa wale wenye uelewa mdogo ambao wanahitaaji kuelezwa ana kwa ana.

Kuhusu namba ya serikali ya kupiga kwa lengo ya kutoa taarifa kwa watu wenye maambukizi au wenye dalili alisema kuwa kwa watu wenye ulemavu wa kutokusikia namba hiyohaiwezi kuwasaidia kwani wao hawapigi simu bali wanatuma ujumbe mfupi.

Akizungumzia uvaaji wa barakoa, Amina alisema viziwi wanapata taarifa kwa kuangaliana midomo kwani wanajua kupitia midomo na mikono sasa kama watavaa barakoa tayari hawawezi kupata ujumbe ambao wanastahili kuupata hasa pale wanapohitaji kupata huduma muhimu.

“Sisi viziwi tunapata ujumbe kwa kutumia alama na kusoma midomo kama tutavaa barakoa tayari hatuwezi kuelewa kinachozungumzwa kwa maana hiyo uvaaji wa barakoa kwetu ni changamoto na ni jambo gumu kwetu,” alisema Amina.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!