May 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Babu mbaroni kwa kubaka mtoto

Nyundo ya Hakimu

Spread the love

JESHI la Polisi mkoa wa Kinondoni linamshikilia Mohamed Hassani (65) mkazi wa Mburahati jijini Dar es Salaam, kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi Kinondoni, Jumanne Muliro amesema tukio hilo lilitokea tarehe 31 Oktoba 2018 ambapo mtuhumiwa huyo anadaiwa kumfanyia ukatili huo mtoto akiwa katika chumba chake.

Kamanda Muliro amesema Jeshi la Polisi linashughulikia tukio hilo kwa mujibu wa sheria na kwamba uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Naye mama mlezi wa mtoto huyo, Hadija Saidi alieleza kuwa, mtuhumiwa huyo ambaye ni mpangaji mwenzie, alimwita mtoto wake chumbani kwake na kumtuma dukani akamnunulie dawa na pipi, na kwamba baada ya mtoto huyo kumletea alivyomtuma, alimfanyia ukatili huo.

error: Content is protected !!