September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Amuua mama yake, anywa damu yake

Spread the love

DANIEL Emanuel (32), mkazi wa Arusha, Sakila katika Wilaya ya Arumeru, amekuta akinywa damu ya mama yake Eliyamulika Emmanuel Sarakikya (79) baada ya kumuua. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha…(endelea).

Taarifa zinaeleza, Daniel alimuua mama yake kwa shoka na kisha akatenganisha, kichwa, mkono, miguu na kiwiliwili chake, akakinga damu ya mama yake kwenye kikombe na kunywa.

Akizungumzia tukio hilo Jonathan Shana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha amesema, mauaji ya mama huyo yamefanywa saa 9 alasiri tarehe 15 Mei 2020, katika Kijiji cha Sakila, Kata ya Kikatiti, King’ori wilayani Arumeru.

Kamanda Shana amesema, wakati Daniel akifanya tukio hilo, majirani walishuhudia akinywa damu ya mama yake baada ya kumuua.

“Daniel alimkata mama yake kwa shoka shingoni na kisha kutenganisha na kiwiliwili chake. Akaona haitoshi, akaanza kukata mguu wa kulia, akakata wa mguu wa kushoto na mkono. Wakati anafanya unyama huu, alikuwa anakinga damu kwenye kikombe anakunywa,” amesema.

Amesema, polisi walipopata taarifa kutoka kwa majirani, walifika haraka kwenye eneo la tukio na kumkuta Daniel akiendelea kunywa damu, na alipowaona alijaribu kukimbia.

“Alipotuona alijaribu kukimbia lakini tulifanikiwa kumkamata,” amesema Kamnda Shana na kuongeza “tumemweka mahabusu hadi upelelezi utakapokamilika.”

Amesema, taarifa za awali zinadai, Daniel ana matatizo ya akili. Licha ya taarifa hizo za awali kutoka kwa baadhi ya watu, Kamanda Shana ametilia mashaka hasa akizungatia maandalizi yaliyofanywa na Danile kabla ya mauaji.

“Hili sikubaliani sana sababu aliwezaje kuandaa shoka, mazingira tulivu yasio na watu pia kwanini kama hana akili alikimbia polisi alipowaona,” amehoji.

 

error: Content is protected !!