Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Ajiua kwa risasi kisa viroba kukamatwa
Habari Mchanganyiko

Ajiua kwa risasi kisa viroba kukamatwa

Pombe aina ya Viroba zikiwa zimekamatwa
Spread the love

FESTO Msalia mfanyabiashara wa vinywaji mkoani Dodoma amejiua kwa kujipiga riasasi kichwani kwa madai kuwa ameumizwa na kitendo cha Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kukamta shehena yake ya pombe za viroba alizokuwa akiziuza,anaandika Charles William.

Serikali ya Tanzania imepiga marufuku uuzwaji wa pombe kali aina ya viroba kwa madai kuwa inasababisha uharibifu wa mazingira kutokana na kufungwa katika mifuko ya plastiki. Marufuku hiyo imesababisha hasara ya mabilioni ya fedha kwa wafanyabiashara wengi.

Tarehe 03 Machi mwaka huu ikiwa ni siku mbili baada ya serikali kuanza operesheni ya kukamata pombe aina ya viroba, Festo anayefanya biashara zake eneo la Dodoma Mjini alikamatwa akiwa na shehena ya tani 1.5 ya pombe hizo, ambzo sasa zinashikiliwa na polisi.

“Alijiua kwa risasi eneo la Veyula, nje kidogo ya mji wa Dodoma. Polisi walipata taarifa na walipoenda eneo la tukio waliokota maganda matano ya risasi na kumuwahisha hospitali mfanyabiashara huyo hata hivyo alikuwa tayari amefariki,” ameeleza Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.

Serikali imekuwa ikilaumiwa kwa kutoa amri ya ghafla ya kupiga marufuku uuzwaji wa pombe za viroba bila kuzingatia kiasi cha ukubwa wa mzigo ambao wafanyabiashara hiyo walikuwa nao. Imekuwa ikielezwa kuwa kitendo hicho kinaweza kuwakatisha tama wawekezaji hapa nchini.

Serikali pia imekata kutoa ruhusa kwa wafanyabiashara hao kuzifunga upya pombe hizo katika chupa ikiwa sababu kuu ya marufu yao ni uchafuzi wa mazingira kupitia mifuko ya plastiki. Imekuwa ikilitumia jeshi la polisi kukagua madukani na kukamata pombe hizo pamoja na wafanyabiashara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!