December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Afisa Usalama (feki) aliyetaka kumtapeli DC Jokate mbaroni

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) inamshikilia Omary Chuma (55) Mkazi wa Chamazi, Temeke Dar es Salaam, aliyejifanya kuwa ni Afisa wa Serikali wa Usalama Taifa na kupanga kumtapeli Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegero. Anaripoti Hamisi Mguta … (endelea).

Ali Mfuru, Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi, (Takukuru), amesema kuwa tapeli huyo alikamatwa tarehe 2 Julai, 2019, baada ya Takukuru kupokea taarifa kuwa mtuhumiwa huyo alifika katika ofisi ya Jokate kwa ajili ya kumtapeli kwa kujifanya kuwa ni Afisa wa Usalama. 

“Uchunguzi wetu umebaini kuwa matapeli hawa wana mtandano mkubwa unaojumuisha watu kutoka ofisi mbalimbali zikiwemo za Serikali, kwa mara nyingine tunatoa agizo na karipio kupitia vyombo vya habari kuwataka waache tabia hii kwani tunayo mamlaka kisheria kuwachukulia hatua,” amesema.

Mfuru amesema kuwa kwa kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa akiwa Wilaya ya Kisarawe atafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Pwani Julai 10, 2019 ili kujibu mashtaka yanayomkabili.

error: Content is protected !!