Tuesday , 21 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi
Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the love

 

JACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza, kwa tuhuma za kumchoma visu hadi kumuuwa mke wake, Mariam Ulacha (42), chanzo kikiwa na wivu wa mapenzi akimtuhumu kuwa na mahusiano na wanaume wengine mahali wanapoishi wilayani Buchosa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mwanza, Wilbroad Mutafungwa, amedai mtuhumiwa alifanya mauaji hayo baada ya kuzozana na marehemu mke wake usiku kucha, kisha asubuhi kuamua kumchoma visu mwilini kitendo kitendo kilichofanya Mariam kuvuja damu hadi kupoteza maisha.

“Mwanaume huyo mkatili alimuuwa mke wake kwa kumchoma visu mwilini mara kadhaa jambo ambali lilipelekea mwanamama huyo kuvuja damu nyingi na hatimaye kupotez amaisha.Chanzo ni wivu wa mapenzi kwa sababu siku moja kabla ya mauaji hayo mwanaume alianza kumtuhumu mwanamke kwa kuwa na mahusiano na wanaume wengine hapo kijijini hali iliyoleta mzozo usiku kucha hatimaye asubuhi akafanya ukatili wake,” amesema Kamanda Mutafungwa.

Kamanda Mutafungwa amesema, baada ya mtuhumiwa kugundua anafuatiliwa kila kona, mnamo tarehe 13 Aprili 2024, aliamua kujisailimisha kwenye Kituo cha Polisi Buchosa.

“Baada ya msako kuwa mkubwa kila eneo analoenda anakuta watu wamejipanga kumkamata aliamua kwenda kujisalimisha kituo cha polisi. Askari wetu waliokuwa kituoni Buchosa walimkaribisha kwa kumfunga pingu na kumueweka chini ya ulinzi ambapo sasa hivi anaendelea kuhojiwa,” amesema Kamanda Mutafungwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Geita, Mwanza waongoza kwa mbwa

Spread the loveNaibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yapata idhini kuwa wakala wa madalali wa DSE

Spread the loveBenki ya NMB imepata idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Waziri aipongeza NBS kwa mafanikio

Spread the loveNaibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande amepongeza Ofisi ya Taifa...

error: Content is protected !!