Wednesday , 22 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Vilio vyatawala miili ya wanafunzi wanafunzi ikiagwa Arusha
Habari za SiasaTangulizi

Vilio vyatawala miili ya wanafunzi wanafunzi ikiagwa Arusha

Spread the love

HUZUNI na vilio vimetawala kwa maelfu  ya waombolezaji wakiwemo familia waliokusanyika leo Jumapili katika shule ya seokondari ya Sinon jijini Arusha kuaga miili tisa ya watu waliofariki katika ajali ya kusombwa na maji jiji Arusha. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Miongoni mwa waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea tarehe 12 Aprili mwaka huu ni wanafunzi nane wa shule ya msingi ya Ghati Memorial katika eneo la Engosengiu kata ha Muriet Jijini Arusha pamoja na muokoaji mmoja.

Askofu Mkuu Isaack Aman wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha anaongoza ibada ya kuuagwa kwa miili hiyo na kutoa baraka kwa ajili ya maziko.

Taarifa za awali zilisema kuwa basi hilo la shule lenye namba za usajili T496 EFK, lilikuwa limebeba wanafunzi 11, walimu wawili na dereva.

Mashuhuda wa tukio hilo wamedaikuwa dereva wa basi hilo la shule alikuwa ametahadharishwa kutovuka eneo hilo lakini akawapuuza.

Watoto wanne waliokuwepo ndani ya basi hilo pamoja na walimu wawili waliokolewa.

Hayo yanajiri wakati mvua kubwa inaendelea kunyesha sehemu nyingi nchini na kusababisha mafuriko maeneo mbalimbali ikiwamo Morogoro na Pwani ambako kumetokea vifo zaidi ya 28.

Miundombinu pia omeharibika okiwamo kukatila kwa barabara na madaraja.

Miili ya wanafunzi wanaoagwa leo Jumapili ni Winfrida Emanuel aliyekuwa anasoma awali, Abigail Peter  darasa la sita, Abialbol Peter (awali), Morgan Emanuel (awali), Articia Emanuel darasa la tatu, Shedrack Emanuel  darasa la sita, Dylan Jeremiah, Noela Jonas (awali) na Brian Tarangie.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaKimataifaTangulizi

Waliowekewa damu yenye VVU, homa ya ini kulipwa fidia trilioni 32.9

Spread the loveWaziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak ameahidi kulipa fidia ya...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yanawa mikono fidia Kimara-Kibamba

Spread the loveSERIKALI imewataka waathiriwa wa bomoabomoa ya upanuzi wa barabara ya...

Habari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

Habari za SiasaKimataifa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

error: Content is protected !!