Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mvua yaua 15 ndani ya wiki moja
Habari MchanganyikoTangulizi

Mvua yaua 15 ndani ya wiki moja

Spread the love

WATU 15 wamefariki dunia kuanzia tarehe 1 hadi 7 Aprili 2024, kwa kusombwa na maji ya mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini huku wengine pia wakipoteza maisha wakiwa wanaogelea. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wengine wamefarika wakiwa wanavuka maeneo ambayo maji yanatiririka kwa kasi na wengine kwa kutumbukia kwenye mashimo ya madimbwi yaliyojaa maji.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu na Msemaji wa Jeshi la Polisi – DCP David Misime imesema miongoni mwa watu hao, watoto ni 12 na watu wazima ni watatu.

Misime amesema matukio hayo yametokea katika wilaya ya Kalambo mkoa wa Rukwa ambapo mtu mmoja mwanaume miaka 18, alisombwa na maji ya mvua yaliyokuwa yakitokea milimani wakati akijaribu kuvuka daraja tarehe 1 Aprili 2024.

Tarehe hiyohiyo katika wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi watoto wawili wote wakiwa na miaka 12 walifariki kwa maji baada ya kusombwa na maji ya mvua.

Tarehe 2 Aprili 2024 mwanaume mmoja wa miaka 28, huko katika Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe alikufa baada ya kufukiwa na udongo ulioporomoka kutokana na mvua kubwa zilizokuwa zinanyesha.

Tarehe 3 Aprili 2024 huko Wilayani Muheza Mkoa wa Tanga, mtoto wa miaka nane alikufa maji wakati akiogelea.

Mkoani Pwani tarehe 3 Aprili 2024 Wilaya ya Mkuranga mtoto mmoja wa miaka 10 alifariki dunia akiogelea mto Mzinga na Wilaya ya Kibaha mtoto wa miaka 12 alikufa maji yaliyokuwa yamejaa katika bonde la mpunga.

Tarehe 5 Aprili 2024 mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 55 huko Wilayani Babati mkoani Manyara alikufa maji baada ya kutumbukia kwenye shimo lenye maji.

Aidha, tarehe 7 Aprili 2024 huko katika Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya watoto watano wenye umri kati ya miaka mitano na sita walifariki dunia baada ya kuzama kwenye dimbwi lilojaa maji ya mvua wakiwa wanaogelea.

Pia tarehe hiyo hiyo huko Mmkoani Geita watoto wawili wenye umri wa miaka tisa na 14 walifariki dunia baada ya kusombwa na maji ya mvua yaliyokuwa yanatiririka kutoka milimani wakitoka kuokota kuni.

“Kutokana na mtiririko wa matukio hayo kwa mwezi huu katika kipindi kifupi na uzoefu wa matukio mengine kama haya ya siku za nyuma linaendelea kutoa wito na tahadhari kwa watu wote hususani wazazi na walezi kuwalinda watoto kwa karibu na kuwapa maelekezo sahihi kutokana na mvua hizi zinazoendelea kunyesha.

“Pia Viongozi wa serikali za mitaa, walimu mashuleni, viongozi wa dini tuendelee kuelimisha watoto wetu kujihadhari na maji yaliyotuama au yanayotembea na wala wasishindane na maji ya mvua yanayotiririka kwani ni hatari kwa maisha yao,” amesema.

Amesema kila mmoja kwa nafasi yake akemee anapoona watoto wakicheza, wakipita au kuogelea kwenye maeneo hatarishi.

Pia sehemu ambazo zinastahili kuwekwa alama za tahadhari ziwekwe au kufunikwa kwa mfano mashimo yaliyochimbwa kwa ajili ya visima vya maji majumbani na sehemu zingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara yaomba bajeti ya Sh. 67.9 bilioni, wamachinga watengewa bilioni 10

Spread the loveBAJETI ya Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Migogoro ya ndoa yaongezeka, Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveMIGOGORO ya ndoa na familia imeongezeka kwa asilimia 8.3  kutoka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yahamasisha uanzishaji vituo vya kulea watoto wachanga

Spread the loveSERIKALI imewahimiza wananchi kujenga vituo vya kulelea watoto wadogo na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

error: Content is protected !!