Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CDF Mabeyo: Magufuli alijua anakufa
Habari za SiasaTangulizi

CDF Mabeyo: Magufuli alijua anakufa

Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati John Magufuli
Spread the love

 

ALIYEKUWA Mkuu wa Majeshi nchini (CDF), Jenerali Venance Mabeyo, amesema Hayati Dk. John Magufuli, alijua kama siku zake za kuishi duniani zimekisha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Jenerali Mabeyo ametoa kauli hiyo katika mahojiano yake na Televisheni ya Mtandao ya Daily News, akizungumzia kumbukumbu ya miaka mitatu ya kifo Cha Hayati Magufuli, kilichotokea tarehe 17 Machi 2021.

Amesema baada ya Hayati Magufuli aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania, kuona Hali yake kiafya sio nzuri aliomba aondolewe katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu kisha arejeshwe akafie nyumbani.

“Siku moja kabla ya kifo chake hali ilibadilika kidogo na yeye alijitambua kwamba hali imebadilika, na nadhani alijua Mwenyezi Mungu alimuongoza kwamba hatapona alichosema nirudisheni nyumbani nikafie nyumbani nikasema mheshimiwa hapana hapa upo kwenye mikono salama madaktari wapo waendelee kukutibu,”amesema Jenerali Mabeyo.

Ameongeza “niseme jambo moja ambalo halikuwahi kusemwa huko nyuma kwa sababu nilikuwepo pale aliniita CDF njoo akaniambia siwezi kupona ,waamuru hawa madaktari wanirudishe nyumbani nikamwambia mheshimiwa sina mamlaka hayo, akasema yaani CDF unashindwa kuwaamuru madaktari wanirudishe nyumbani, nikamwambia suala la afya siyo la CDF mheshimiwa naomba ubaki utulie madaktari watatuambia.”

Jenerali Mabeyo amesema baada ya kukataa ombi hilo, Hayati Magufuli alimuomba amuitie viongozi wa dini Kwa ajili ya kumfanyia maombi ya mwisho.

“Alipoona nimekuwa na msimamo huo akaniambia niitieni paroko wangu wa St. Peters, Father Makubi, akaongeza akasema namuomba Kadinali Pengo naye aje hiyo ni asubuhi…Kwa hiyo wakajs wote sasa katika taratibu za kikatoliki wanamsalia ibada ya kumpa sakramenti ya upako wa mgonjwa aliyekuwa katika hatari ya kufariki. Walipomaliza kumsakia akapumzika lakini ilipofika mchana Hali yake ilibadilika tukaenda tukamkuta ametulia lakini hawezi kiongea Tena tukaendelea kukaa mpaka jioni saa 12 akafariki Dunia,” amesema Jenerali Mabeyo.

Amesema ficho cha Hayati Magufuli aliyefariki akuwa madarakani, kilichelewa kutangazwa ili kupata muda wa kuipa taarifa familia yake hasa mama yake mzazi aliyekuwepo kijijini kwao Chato mkoani Geita.

Amesema baada ya kifo hicho kutokea, walizingatia matakwa ya katiba katika mchakato wa mabadiliko ya kiongozi Kwa kumuapisha aliyekuwa makamu wake wa Rais, Samia Suluhu Hassan, kurithi mikoba yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!