Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bodi mpya NEEC yapewa ujumbe mzito
Habari Mchanganyiko

Bodi mpya NEEC yapewa ujumbe mzito

Spread the love

NAIBU Waziri  wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ummy Nderiananga amewataka wajumbe wa Bodi ya Saba ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC) kuwa wabunifu sambamba na kuzingatia uadilifu na uweledi  ili kuchochea wananchi kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo chini ya Uenyekiti wa Profesa Aurelia Kamuzora Jijini Dar es Salaam, Waziri Nderiananga  amesema Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Na. 16 ya mwaka 2004 imeipa bodi mamlaka ya kusimamia baraza, ili liweze kufikia malengo  ya Serikali ikiwemo kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake.

“Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imewaamini hivyo jukumu lenu ni kuonesha mchango  stahiki ikiwa ni pamoja na kusimamia utendaji wa baraza.

Naamini kwa umoja wenu na ushirikiano na menejimenti ya NEEC mtaweza kufanikisha hili na kuleta  matokeo chanya katika kukuza uchumi wa Taifa,” amesema  Waziri Nderiananga.

Amesema mafanikio ya NEEC yanategemea kwa kiasi kikubwa miongozo na utendaji wa bodi, ili  kuibua na kubuni mbinu zitakazoweza kutanua wigo wa utoaji huduma za uwezeshaji kwa weledi na kufikia wananchi wengi nchini.

“Bodi hii inatarajiwa kutekeleza majukumu yake kwa kipindi cha miaka mitatu, hivyo ni jukumu la bodi kuhakikisha baraza linafikia malengo na matarajio ya wananchi katika kipindi chote cha utendaji wake” amesisitiza Nderiananga.

Aidha, ameipongenza menejimenti ya NEEC  kwa utekeleza na kufikia malengo ya kuundwa kwa  baraza hivyo ni imani yake kuwa bodi mpya itapata ushirikiano mkubwa.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa NEEC,  Bengi Issa, ameahidi kuwa menejimenti yake  kwa kushirikiana na wadau watafanya kazi kwa karibu  na bodi,  ili kufikia azma ya Serikali ya kukuza ushiriki wa Watanzania kwenye shughuli za kiuchumi pamoja na manunuzi ya umma hususa makundi maalum (wanawake, vijana, wazee na watu wenye ulemavu).

“Sisi kama baraza tutaendelea kuratibu wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusimamia mifuko ya uwezeshaji ambayo mpaka sasa tunayo mifuko 72 ambapo 62  ipo ndani ya Serikali na  10 hipo nje ya Serikali, lakini tunairatibu na kuhakikisha tunapata taarifa ya utekelezaji wao,” amesema Issa.

Amesema baraza  limejipanga kuendelea kuwajengea uwezo watanzania  ikiwa ni pamoja na kuendesha mafunzo nchi nzima  yatakayo angazia namna bora ya  kutumia   mifumo iliyoanzishwa na  serikali  sambamba na  kufanya urasimishaji wa biashara ili ziwe rasmi.

Naye Mjumbe wa Bodi iliyomaliza mda wake,   Profesa Lucian Msambichaka alisisitiza bodi mpya kufanya kazi kwa umoja ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu yao kwa kuzingatia Sera, Sheria na Kanuni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!