Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri mkuu atoa agizo wasimamizi mji wa serikali
Habari za Siasa

Waziri mkuu atoa agizo wasimamizi mji wa serikali

Spread the love

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wasimamizi na wataalamu wa ujenzi wa Mji wa Serikali jijini Dodoma wahakikishe matarajio ya ujenzi huo yanafikiwa kama ilivyokusudiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na Mtawala wa Mamlaka ya Kusimamia Uendelezaji wa Mji wa Serikali wa Korea Kusini, HyeongRyeol Kim.

Amekutana na kiongozi huyo leo Ijumaa katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni Jijini Dar es Salaam, baada ya hafla ya utiaji saini mikataba ya makubaliano kati ya taasisi za Korea Kusini na Tanzania.

Makubaliano hayo yanahusu kubadilishana uzoefu juu ya usimamizi na uratibu wa uendelezaji wa makao makuu na mji wa Serikali pamoja masuala ya ujenzi vikiwemo viwanda, hoteli.

Utiwaji saini huo umefanyika kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi Uendelezaji wa Mji wa Segong na kampuni ya Heerim ya Korea Kusini katika masuala ya usanifu na ubunifu wa ujenzi kwenye Mji wa Serikali na Makao Makuu jijini Dodoma.

“Serikali ya Tanzania na Korea Kusini zina mahusiano mazuri ya kidiplomasia, hivyo matarajio yetu ni kuona Makao Makuu na Mji wa Serikali jijini Dodoma unakuwa mzuri.”

Kwa upande wake, HyeongRyeol Kim amesema utiaji saini wa makubaliano hayo ni fursa muhimu ya kuendeleza ushirikiano baina ya mataifa hayo.

Pia, Kim amemshukuru Waziri Mkuu kwa mapokezi mazuri aliyoyapata na amemuhakikishia kwamba nchi yao itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuliendeleza jiji la Dodoma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!