Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Akina Dk. Slaa wataka uchaguzi serikali mitaa usogezwe mbele kupata katiba mpya
Habari za Siasa

Akina Dk. Slaa wataka uchaguzi serikali mitaa usogezwe mbele kupata katiba mpya

Spread the love

TAASISI ya Sauti ya Watanzania imeshauri uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwaka huu, usogezwe mbele hadi uchaguzi mkuu wa 2025, ili kupata muda wa kukamilisha mchakato wa upatikanaji katiba mpya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa na taasisi hiyo wakati wajumbe wake, akiwemo Dk. Wilbroad Slaa, Askofu Emmaus Mwamakula na Wakili Boniface Mwabukusi, wanazungumza na waandishi wa habari leo tarehe 8 Januari 2024, jijini Dar es Salaam, kuhusu miswada ya marekebisho ya uchaguzi iliyowasilishwa bungeni mwaka jana.

Wakili Mwabukusi amedai kuwa muda wa kukamilisha mchakato huo unatosha kwa kuwa kazi kubwa ilishafanyika na kwamba zoezi hilo linaweza kufanyika ndani ya miezi mitatu.

“Kwa kuwa jambo si gumu sababu asilimia kubwa ya wale watu walioshiriki kukusanya maoni ya wananchi wapo na wengine wapya wapo, utengenezwe utaratibu wa sheria ihuishwe na kwa kuisoma hii katiba yetu Rais ana mamlaka wanaweza kusogeza mbele uchaguzi wa serikali za mitaa ili uchaguzi wote ufanyike pamoja mwakani na hilo linawezekana.

“Kinachotakiwa sasa ni utungwaji wa sheria kukwamua pale Mzee Warioba alivyopigwa sarakasi bunge la katiba likakusanya maoni ikaja katiba pendekezwa, pale ndipo penye mkwamo na hiyo kazi ukiwapa watu makini wenye uchungu na nchii inahitaji miezi mitatu tu kuunganisha maeneo gani yenye shida,” amesema Mwabukusi.

Wakili Mwabukusi amedai kuwa, katiba ya sasa haihitaji marekebisho madogo kwa kuwa ina viraka zaidi ya 14 hivyo inapaswa kuandikwa upya, huku akidai inatakiwa katiba mpya iwabane viongozi kuwatumikia wananchi wanaowachagua.

Kwa upande wake Askofu Mwamakula, amesema kwa sasa Bunge limebeba dhamana ya kufanyia kazi maoni na mapendekezo ya wananchi yaliyoachwa, kwa kuhakikisha yanajumuishwa ili sheria zitakazotungwa zikidhi matakwa yao.

“Miswada iko chini ya kamati ya bunge, ina wajibu mkubwa kusikiliza maoni hayo, kuyachambua na kuangalia yale yenye maslahi mapana kwa taifa wayachukue. Nafasi ipo kwa wabunge kuhakikisha kile kinachopita ni maoni ya wananchi lakini serikali ina nafasi kama imeona kuna namna yoyote huwezi kurekebisha wanayo nafasi ya kuiondoa bungeni waiandae upya,” amesema Askofu Mwamakula.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RUWASA yachongewa, yateketeza mamilioni kwa maji yenye magadi

Spread the loveSAKATA la ukosefu wa maji wilayani Momba mkoani Songwe limezidi...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

error: Content is protected !!