Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Puma energy Tz yakabidhi msaada wa mil. 70 Hanang
Habari Mchanganyiko

Puma energy Tz yakabidhi msaada wa mil. 70 Hanang

Spread the love

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania imekabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi zikiwemo nondo 1000, mabati 800 pamoja na saruji mifuko 600 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko ya matope yaliyotokea Kateshi wilayani Hanang mkoani Manyara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara…(endelea).

Vifaa hivyo vya ujenzi vyenye jumla ya thamani ya Sh.milioni 70 vimekabidhiwa leo tarehe 28 Desemba 2023 wa Serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Hanang mkoani Manyara, Janeth Mayanja.

Mkuu wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Janeth Mayanja (wa pili kulia )akipokea mfuko wa saruji ukiwa ni sehemu ya mifuko 600 ya saruji kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania ambaye ni Meneja Uhusiano Godluck Shirima( wa tatu kushoto) Meneja Masoko Lilian Kanora(wa kwanza kulia) na Meneja Rasilimali Watu, Joseph Jaruma ( wa pili kushoto).Wa kwanza kulia ni Ofisa Ugavi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Methew Giramisi.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja ameishukuru Kampuni ya Puma Energy Tanzania kwa kutoa vifaa vya ujenzi ambavyo kwa sasa ndivyo vinahitahika zaidi.

“Kwa niaba ya Serikali anachukua nafasi hiyo kuupongeza uongozi wa Puma Energy Tanzania kwa kufika Kateshi kutoa misaada wa vifaa vya ujenzi. Tumepokea mifuko ya saruji 600, bati pisi 800 na nondo 1000.

“Vifaa hivi vya ujenzi vitasaidia eneo la ujenzi  kwani tunakusudia kuanza ujenzi hivi karibuni kujenga nyumba za waathirika wale ambao wamepoteza makazi na mchango huu una  thamani ya Sh. milioni 75,” amesema Mayanja.

Mkuu wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Janeth Mayanja (wa tatu kushoto) akipokea bati kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania ambaye ni Meneja Uhusiano Godluck Shirima( wa pili kulia).Wanaoshuhudia Meneja Masoko Lilian Kanora(wa pili kushoto) na Meneja Rasilimali Watu, Joseph Jaruma (wa kwanza kulia). Wa kwanza kushoto ni Ofisa Ugavi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang mkoani Manyara Methew Giramisi.

Ameongeza kuwa msaada huo wa  nondo, bati na saruji unakwenda kuongeza nguvu katika jitihada za Serikali za Awamu ya Sita chini ya ya Samia Suluhu Hassan ambayo imeamua kujenga nyumba kwa waathirika baada ya kutokea mafuriko tarehe 3 Desemba 2023

Aidha, amesema msaada huo umekuja wakati muafaka kwani wamekuwa wakipokeza zaidi msaada wa mahitaji ya chakula na dawa lakini kwa sasa wako kwenye hatua za mwisho kuanza ujenzi wa nyumba za waathirika kwa kutambua baada ya mafuriko kuna baadhi ya makazi yameharibiwa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Fatma Mohemed Abdallah, Meneja Uhusiano wa Puma Energy Tanzania Limited Godluck Shirima amesema bodi ya wakurugenzi chini ya Mwenyekiti wake Dk. Selemani Majige, Menejimenti ya Kampuni chini ya uongozi wa Fatma Mohamed Abdallah, wafanyakazi na wadau wote wameguswa na kuhuzunishwa na mafuriko yalio wakuta wananchi wa Katesh.

“Hivyo viongozi wetu wakatuelekeza kuleta msaada huu wa vifaa vya ujenzi ili kuunga mkono juhudi na jitihada za Serikali kuwajengea makazi waathirika waliopoteza makazi yao kwenye mafuriko.

“Puma Energy pia ni muathirika wa mafuriko haya, ambapo kituo chao cha Kateshi kiliharibiwa na mafuriko, kwa hiyo kama waathirika na mkazi wa Kateshi, kampuni iliona ni vyema kutoa mchango wake kwa jamii ya Katesh,” amesema Shirima.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!