Tuesday , 14 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rombo yafurika, LATRA watoa watoa vibali vya muda
Habari Mchanganyiko

Rombo yafurika, LATRA watoa watoa vibali vya muda

Spread the love

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) mkoa wa Kilimanjaro, imelazimika kutoa kibali kwa mabasi madogo ya abiria maarufu kama Coaster  ya  kukodi “special hire” ili kubeba abiria kuelekea wilaya ya Rombo kutokana na wingi wa abiria.

Wingi huo wa abiria unatakwa kusababisha uhaba mkubwa wa usafiri kwenye njia  hiyo janq Jumapili. Anaripoti Safina Sarwatt, Kilimanjaro…(endelea).

Mamlaka hiyo ilifanya ukaguzi kwa njia zote na kuelekeza mabasi kutoa kibali kwenye  njia zenye uhitaji wa abiria wengi na kuchukua hatua kwa gari za ruti kuzidisha nauli na kuvunja sheria ya usafirishaji.

Akizungumzia adha hiyo kwa waandishi wa habari Afisa mfawidhi mamlaka ya udhibithi usafiri ardhini LATRA mkoa wa Kilimanjaro, Paul Nyello amesema katika kipindi hiki cha sikukuu ya krimasi kuanzia tarehe 23-24 Desemba, abiria ni wengi na magari hayatosheleza mahitaji.

” Tarehe 23 na 24 abiria walizidi kushinda uwezo wa mabasi ya njia za Rombo na Tarakea ambapo ndipo kuna abiria wengi zaidi hali iliyolazimu mamlaka kuchukua hatua kwa magari makubwa kama coaster za kukodi maarufu special hire  na kupatana bei nafuu kwa abiria ,”amesema Nyello

“Mabasi makubwa ya masafa marefu kama Ngasere yalitoa huduma  pia,”

Amesema kuwa magari ya kukodi special hire yalitakiwa kuwabeba abiria katika njia hiyo kwa bei ya kupatana kwani yale magari yanasheria zake na utaratibu hasa ikizingatiwa yapo kwa ajili ya kukodiwa.

Amesema mamlaka ikishirikiana na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani walikuwa stendi na kuhakikisha abiria wote wanapata usafiri.

Amesema kuwa mamlaka hiyo pia ilifanya ukaguzi kwenye magari yote ya ruti za ndani na kuhoji abiria kama wamezidishiwa nauli lakini hakukuwa na abiria yoyote aliyelalamika.

Nao baadhi ya abiria wakizungumza kwa nyakati tofauti na wandishi wa habari wameshukuru LATRA kwa kusimamia vema suala la nauli na kuwasaidia kuwapatia usafiri kutokana magari katika njia Rombo Tarakea kutosheleza mahitaji yote ya abiria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaBiasharaHabari Mchanganyiko

EXIM Bank, Msalaba Mwekundu wapanda miti, wachangisha damu

Spread the love  BENKI ya Exim imeshirikiana na Chama cha Msalaba Mwekundu...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Bunge lakemea utoroshwaji mifugo kuelekea Kenya

Spread the loveKamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na...

ElimuHabari Mchanganyiko

Waziri SMZ akoshwa na kazi za Global Education Link

Spread the loveSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar SMZ imesema itaendesha msako na kuzifutia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CUF yajipanga kuelekea chaguzi zijazo

Spread the loveCHAMA cha Wananchi (CUF), kimejipanga kujijenga kisiasa kuelekea chaguzi zijazo...

error: Content is protected !!