Saturday , 18 May 2024
Home Habari Mchanganyiko SUKITA yatumia michezo kufikisha elimu ukatili kwa jamii
Habari Mchanganyiko

SUKITA yatumia michezo kufikisha elimu ukatili kwa jamii

Spread the love

SHIRIKA la Usawa wa Kijinsia Tanzania (SUKITA), limeamua kutumia michezo kama mbinu ya kufikisha elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia kwa jamii. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea)

Akizungumza katika bonanza la michezo lililofanyika jana Jumapili  kwenye Uwanj wa Barcelona, Mabibo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa SUKITA, Msafiri Mwajuma Mariam, alisema wameamua kutumia mbinu hiyo ili kufikia watu wengi zaidi.

Msafiri alisema kuwa, kabla ya kutumia mbinu ya michezo walianza kwenda katika nyumba za ibada pamoja na shule, ili kuzungumza na wananchi juu ya athari za ukatili wa kijinsia na namna ya kuripoti matukio hayo kwenye vyombo vya dola kwa ajili ya wahusika kuchukuliwa hatua.

“Tunafanya yote haya kwa udhamini wa Mfuko wa Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Tanzania (WFT-T), ambapo tulianza kwenda shuleni, kanisani na misikitini kuzungumza na wananchi ili ujumbe ufike kwenye jamii ya chini. Tumeamua kutumia michezo kwa kuwa inapendwa sana hivyo huwakusanya watu wengi ambapo tunapata nafasi ya kuwapa elimu,” alisema Msafiri.

Mbali na kufikisha elimu kwa jamii, Msafiri alisema SUKITA imefanikiwa kushawishi uundwaji wa kamati za utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), ngazi ya mtaa na kata, kwenye wilaya ya Ubungo na Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

“Tangu tuhamasishe uundwaji wa kamati za MTAKUWWA ukatili umepungua wananchi wanaripoti matukio lakini changamoto tunayokabiliana nayo ni wananchi kutelekeza kesi, wakisharipoti polisi wakiambiwa wakatoe ushahidi mahakamani wanaingia mitini,” alisema Msafiri.

Bonanza hilo lilihudhuriwa na watu mbalimbali, ikiwemo viongozi wa MTAKUWWA ngazi ya mtaa, polisi kutoka madawati ya jinsia, viongozi wa dini na vyama vya siasa.

Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika SheiRa na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF), Anna Kulaya alisema “leo tumekuja hapa kujadili jinsi gani tutaishirikisha jamii katika utokomezaji ukatili wa kijinsia, ambapo watoa mada mbalimbali watatoa elimu kwa wananchi.”

Kulaya alisema jamii bila ukatili wa kijinsia inawezekana endapo wadau, serikali na wananchi watashirikiana kuvitokomeza.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Chakula Bora, uliopo Kata ya Manzese ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya MTAKUWWA, Odo Ramadhan, alisema kazi zinazofanywa na SUKITA zimesaidia kupunguza ukatili kwenye eneo lake.

“Nawashukuru sana SUKITA sasa hivi ukatili wa kijinsia umepungua na nina hakika kama watakuwa wanatoa semina kama hizi mwisho wa siku Tanzania ukatili wa kijinsia utaisha kabisa,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua bima ya afya kwa wakulima

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni...

Habari Mchanganyiko

Makamba awasili China kwa ziara ya kikazi

Spread the loveWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Ethiopia yafungua njia ujenzi wa ubalozi Dodoma

Spread the loveSerikali ya Tanzania imeipongeza Serikali ya Ethiopia kwa kuweka historia...

error: Content is protected !!