Saturday , 18 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kesi ya mauaji Kakonko kutajwa Desemba 28
Habari Mchanganyiko

Kesi ya mauaji Kakonko kutajwa Desemba 28

Spread the love

KESI ya mauaji inayowakabili maofisa uhamiaji  watatu wilayani Kakonko waliofikishwa kizimbani kwa tuhuma za kumuua Enos Elias itatajwa tarehe 28 Desemba mwaka huu. Anaripori Faki Sosi …(endelea).

Maofisa hao ni pamoja na Joachim Frathazaus (Kafupi), Fredrick Kyomo na Mabrouk Hatibu.

Awali watuhumiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu ya Wilaya ya Kakonko tarehe 28 Oktoba mbele ya Hakimu Kyamba ambapo Charles Mwakanyamale Mwendesha Mashtaka wa Serikali aliwasomea shtaka moja la kufanya mauaji kwa kukusudia

Watuhumiwa hao tarehe 28 Oktoba wanadaiwa walimuua kwa makusudi kijana Enos Elias (20) katika kijiji cha Chilambo.

Kesi hiyo namba 38283 ilitajwa jana tarehe 11 na kuahirishwa mpaka tarehe 28 Desemba 2023 kwa ajili ya kutajwa ambapo upande wa Jamhuri unaendelea na Mashtaka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua bima ya afya kwa wakulima

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni...

Habari Mchanganyiko

Makamba awasili China kwa ziara ya kikazi

Spread the loveWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Ethiopia yafungua njia ujenzi wa ubalozi Dodoma

Spread the loveSerikali ya Tanzania imeipongeza Serikali ya Ethiopia kwa kuweka historia...

error: Content is protected !!