Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Momba wabuni mradi wa mwalo wa samaki Samang’ombe
Habari Mchanganyiko

Momba wabuni mradi wa mwalo wa samaki Samang’ombe

Spread the love

 

HALMASHAURI ya wilaya ya Momba mkoani Songwe,ili kujipatia mapato yake ya ndani imebuni kujenga Mwalo wa Samaki, kwa gharama ya Tshs,1,101,466,162.00 kwa ajili kuongeza ajira kwa vijana na mapato. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe … (endelea). 

Momba inamiliki sehemu ya ziwa Rukwa kwa ukubwa ukubwa wa kilometa za mraba 292 katika kata za Ivuna, Mkomba na Kamsamba hivyo vijiji sita vinapakana na ziwa hillo.vjiji hivyo ni Samang’ombe, Kalungu, Lwatwe, Chole, Siliwiti na Senga.

Akizungumza leo tarehe 14 Novemba, 2023 Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Regina Bieda, amesema ujenzi huo wa mwalo ulisainiwa kati ya uongozi was wizara ya mifugo na uvuvi na mkandarasi kampuni ya Stance  Techinic and Civil Engineering Ltd 25/5/2023.

Alisema mwisho wa utekelezaji wa mradi ni miezi sita na makisio yake ni Tshs, 1,101,466,162.00 na kwamba utakapo kamilika utarahisisha ukusanyaji mapato na kuongeza ajira kwa vijana.

“Mradi ukimamilika utarahisisha ukusanyaji mapato ya mazao ya uvuvi,ukaguzi wa mazao ya uvuvi na kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi, mwalo huo pia utatumiwa na wilaya jirani za Songwe na Sumbawanga,” alisema Bieda.

Alisema miundombinu inayojengwa ni jengo la walinzi, Utawala,eneo la kupakia magari, jengo la vyumba vya ubaridi, jengo la mtambo wa kuzalishia barafu,chumba cha kuhifadhia Samaki, jengo la mama lishe/baba lishe.

Mkurugenzi Mtendaji wa Momba, Regina Bieda

Bieda alitaja majengo mengine kuwa ni jengo la vyoo,eneo la kuchakatia samaki, eneo la kukaushia samaki kwa moshi pamoja na mifumo ya maji safi  na maji taka.

Alitaja idadi ya wavuvi waliopo ni 456,idadi ya wafanyabiashara wa samaki ni 82,idadi ya vyombo vya uvuvi ngalawa 106, mitumbwi 138 ,idadi ya boti za kubebea samaki 4 idadi ya ya akina baba/mama lishe 73.

Aidha Bieda alitaja aina ya samaki na tani wanazovuna gege tani 69.60 mwaka 2021,na tani 76..50 mwaka 2022 na Kambale tani 17.15 mwaka 2021 na tani 21.08 mwaka 2022 huku akitegemea kiwango kuongezeka mwaka huu.

Katibu tawala mkoani humo Happiness Seneda akiwa ziarani kwenye Mradi huo alimtaka mkurugenzi na timu yake kuwasimamia kwa ukaribu wakandarasi wanaojenga mradi huo ili ukamilike kwa wakati na kwa viwango.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!