Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wazee 272 waliopigana vita Kagera waendelea kulipwa pensheni
Habari za Siasa

Wazee 272 waliopigana vita Kagera waendelea kulipwa pensheni

Spread the love

SERIKALI imesema inaendelea kuwalipa pensheni ya ulemavu wazee 272, waliopigana vita ya Kagera 1979. Anaripoti Jemimah Samwel, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamesemwa leo tarehe 9 Novemba 2023, bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax, akimjibu Mbunge Viti Maalum (CCM), Fakharia Shomar, aliyehoji Serikali inatoa kauli gani kuhusu kuwasaidia walioapata ulemavu wakati wa kupigana katika vita hiyo.

Dk. Tax amesema, mbali ya wazee hao kulipwa pensheni, wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye hospitali za jeshi, pamoja na kupata stahiki nyingine kwa mujibu wa sheria ya pensheni na viinua mgongo za mwaka 1966.

“Wengi kati ya wapiganaji hao walipewa ajira katika vyombo vya Ulinzi na Usalama hususani Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza. Aidha, wapo walioshindwa kuajiriwa kutokana na sababu mbalimbali,”alisema Dk. Tax.

Aidha, Dk. Tax amesema wizara yake inaendelea kufuatilia hali zao ili kuchukua hatua stahiki, huku akiwataka wazee ambao hawanufaiki na huduma hizo, kuwasilisha taarifa zao ili wasaidiwe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!