Monday , 20 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mchungaji ataka haki itendeke chaguzi 2024, 2025
Habari za Siasa

Mchungaji ataka haki itendeke chaguzi 2024, 2025

Spread the love

MCHUNGAJI kiongozi wa kanisa la Tanzania Assembles of God (TAG) URCC lililopo Aread D Jijini Dodoma, Salum Vangast ametoa wito kwa mamlaka zote nchini kuhakikisha zinasimamia haki mchakato mzima wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu 2025. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea)

Mchungaji Vangast ametoa wito huo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza Ibada maalumu iliyoambatana na maombi kwa ajili ya kujiweka wakfu yaliyofanyika kanisani hapo na kuongozwa na Makamu Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dk. Magnus Muhiche.

Kiongozi hiyo wa kiroho amesema kanisa limefanya maombi kwa ajili ya kujiweka wakfu na kutenbea upya katika uwepo wa Bwana Yesu kwa lengo la kuliombea taifa pamoja na mataifa mengine ili kurejesha hali ya amani na utulivu pale itakapokuwa imetoweka.

Amesema ili amani na utulivu uwepo lazima watu wawe na hofu ya Mungu na zaidi hofu hiyo itokane na watu kumjua Mungu na kutambua umuhimu wa kutenda haki.

Akizungumzia kuhusu nchi ya Tanzania amesema ni busara kila mmoja kwa nafasi yake akatambua umuhimu na thamani ya haki na kueleza kuwa haki inazaa amani na amani inazaa utulivu.

Kutokana na hali hiyo amesema vyombo vya dola hapa nchini vinatakiwa kuhakikisha vinasimamia haki, amani na utulivu na kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na uchaguzi Mkuu wa 2025.

“Haki inatakiwa kutawala na atakayekuwa ameshinda atangazwe kwa ushindi wake na atakayeshindwa atangazwe kwa kushindwa kwake na si vinginevyo,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Kiongozi Mkuu Iran amteua mrithi wa Rais Ebrahim

Spread the loveKiongozi wa ngazi ya juu nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei,...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 85,471 walioenguliwa kipindi cha JPM wapandishwa vyeo

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa jumla...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

error: Content is protected !!