Monday , 20 May 2024
Home Habari Mchanganyiko RC Dodoma kuongoza usimikwaji wa Askofu mkuu PHC
Habari Mchanganyiko

RC Dodoma kuongoza usimikwaji wa Askofu mkuu PHC

Rosemary Senyamule- Geita
Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule  anatarajiwa kushirikiana na  waumini kutoka madhehebu mbalimbali ya dini katika ibada maalum kusimikwa kwa viongozi wa ngazi ya kitaifa wa Kanisa la The Potter’s House Church.

Ibada hiyo itaenda sambamba na kuhitimishwa kwa Kongamano la Maaskofu linalofanyika kwenye kanisa hilo lenye makao makuu  Mlimwa Kusini Kata ya Ipagala Mkoani Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari Askofu Mkuu Mteule wa Kanisa hilo, Ruth Chilendu  alisema pamoja na mkuu huyo wa mkoa pia viongozi wengine wa kidini wa kitaifa watakaoshiriki kwenye ibada hiyo maalumu ni maaskofu kutoka Marekani, Zambia na Kenya na Wachungaji na waumini kutoka madhhebu mengine.

Askofu Ruth aliwataja viongozi hao ambao watakaosimikwa kwenye ibada hiyo itakayohudhuriwa na viongozi wa serikali wa ngazi vitongoji, mitaa , kata, wilaya hadi  mkoa kutoka mkoani hapa.

Aliwataja viongozi ambao watakaosimikwa kwenye ibada hiyo ni pamoja na nafasi ya Askofu mkuu wa Kanisa hilo, Ruth Chilendu, Makamu Askofu mkuu Jangisi Kolongo, Katibu Mkuu Festo Lesilwa na Mhazini Mkuu Yohana Sudai.

Alisema katika ibada hiyo ambayo itasimamiwa na mmoja wa Maaskofu aliyetajwa kwa jina moja la Askofu Mwakilembe kutoka Mlandizi mkoani Pwani, Askofu Ruth alisema kuwa kusimikwa kwa viongozi hao wa Kanisa hilo ni matumaini yake kuwa linaenda kuhubiri Injili kwa mataifa yote ndani na nje ya mipaka ya nchi.

“Kanisa kwa sasa linaenda kupanua wigo wa kuhakikisha kila mkoa, wilaya, kata vijiji mitaa vitongoji ndani ya nchi tunaenda kuwafikia watu wake kwa kuwapatia huduma ya kiroho na kijamii hii inatokana na malengo ambayo tumejiwekea kwa kushirikiana na serikali kupitia katiba ya nchi”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 85,471 walioenguliwa kipindi cha JPM wapandishwa vyeo

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa jumla...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

error: Content is protected !!