Saturday , 18 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Makamu wa pili wa Rais Zanzibar atembelea banda la GGML maonesho ya madini Geita
Habari Mchanganyiko

Makamu wa pili wa Rais Zanzibar atembelea banda la GGML maonesho ya madini Geita

Spread the love

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman leo Jumamosi ametembelea banda la Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) katika maonesho ya sita ya teknolojia ya madini Geita na kupata maelezo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mgodi huo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Pia amepata maelezo kuhusu huduma za uchunguzi na elimu ya saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume zinazotolewa na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita kwa ushirikiano wa GGML ambapo hadi jana zaidi watu 1000 wamefanyiwa vipimo.

Meneja Mwandamizi wa GGML anayeshughulikia mahusiano ya jamii, Gilbert Mworia akimpatia zawadi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman alipotembelea banda la kampuni hiyo katika Maonesho ya Sita ya Tekonolojia ya Madini Geita. Suleima alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa maonesho hayo.

Akitoa maelezo kwa Makamu Rais huyo wa Zanzibar ambaye ndiye mgeni rasmi anayefunga maonesho hayo yaliyofanyika kwa siku 10, Meneja Mwandamizi wa GGML anayeshughulikia mahusiano ya jamii, Gilbert Mworia alisema kampuni hiyo ndio inayoongoza kwa kuwa muajiri bora nchini.

Pia inaongoza kuwa kuzingatia sheria ya local content Pamoja na kuzingatia masuala ya usalama kazini.

Mkurugenzi mtendaji wa GGML, Terry Strong akimshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman alipotembelea banda la kampuni hiyo katika Maonesho ya Sita ya Tekonolojia ya Madini Geita. Suleima alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa maonesho hayo.

Pamoja na mambo mengine amesema GGML ambaye ni mdhamini mkuu wa maonesho hayo yaliyoanza tarehe 20 Septemba mwaka huu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong amemshukuru Makamu huyo wa Rais kwa kutembelea banda hilo na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua bima ya afya kwa wakulima

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni...

Habari Mchanganyiko

Makamba awasili China kwa ziara ya kikazi

Spread the loveWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Ethiopia yafungua njia ujenzi wa ubalozi Dodoma

Spread the loveSerikali ya Tanzania imeipongeza Serikali ya Ethiopia kwa kuweka historia...

error: Content is protected !!