Saturday , 2 December 2023
Home Kitengo Michezo Waziri madini atembelea banda la GGML, ashuhudia mradi wa uwanja wa kisasa
Michezo

Waziri madini atembelea banda la GGML, ashuhudia mradi wa uwanja wa kisasa

Spread the love

WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde ametembelea banda la Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) katika maonesho ya sita ya teknolojia ya madini Geita na kupata maelezo kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Waziri huyo pia alishuhudia mfano wa mradi wa uwanja wa kisasa wa michezo (Magogo Stadium) unaojengwa na GGML kwa lengo la kuendeleza michezo mkoani Geita.

Akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa GGML, Stephen Mhando alielezwa kwamba kampuni hiyo ambayo imeshiriki mara zote sita tangu maonesho hayo yaasisiwe mwaka 2018, imekuwa mdhamini mkuu na mwaka huu pia imetoa Sh milioni 150.

Mhando alimueleza pia Waziri kuwa mbali na udhamini huo mwaka huu, GGML imetoa jenereta maalumu ili kukabiliana na dharura yoyote ya umeme itakapojitokeza.

Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Stephen Mhando akimpatia maelezo Waziri wa Madini, Anthony Mavunde kuhusu baadhi ya miradi inayotekelezwa na GGML ikiwamo ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Magogo ambao unatakelezwa na kampuni hiyo.

Mbali na Mavunde kutembelea idara tisa za GGML zilizopo katika maonesho hayo, pia Mhando alimueleza kuwa zaidi ya Sh bilioni 2.4 hadi sasa zimetumika katika mradi huo wa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo akimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya GGML alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho hayo ya teknolojia ya madini yanayoendela mjini Geita.

“Kazi hii inaendelea na sisi GGML kama wadhamini wakuu wa Timu ya Geita Footbal Club, tunaamini kuwa uwanja utakapokamilika utakuwa moja ya chanzo cha mapato hata kwa halmashauri ya Geita,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Fernandes hakamatiki Man Utd, mahesabu ni kuifunga Bayern

Spread the love  NAHODHA wa Manchester United, Bruno Fernandes, alikuwa na kiwango...

Michezo

Meridianbet na Ligi ya Europa inakupa pesa za kumwaga mapema sana

Spread the love  KOMBE la UEFA Europa League ni zito kuliko makombe...

Michezo

Kwapua mpunga na mechi za UEFA leo na kesho

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya kuendelea leo na kesho...

AfyaMichezo

GGML yatoa milioni 17 kung’arisha ATF Marathon

Spread the loveKATIKA kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kukabiliana na maambukizi...

error: Content is protected !!