Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko ATCL yataja sababu kusitisha safari za ndege China
Habari Mchanganyiko

ATCL yataja sababu kusitisha safari za ndege China

Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)
Spread the love

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imetoa ufatanuzi kuhusu mabadilko ya ratiba zake za safari za China kwa abiria wake kuwa zimetokana na ndege zote mbili za masafa marefu Boeing 787-7 (Dreamliner) kufikia muda wake wa matengenezo ya kawaida (maintenance schedule). Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasllano kwa Umma kutoka ATCL,  Sarah Reuben, matengenezo hayo yalipangwa kufanyika kwa awamu.

Hata hivyo,  kutokana na kuvurugika kwa mfumo wa ugavi (supply chain) katika utengenezaji wa vipuri vya ndege uliosababishwa na athari za UVIKO 19; ratiba ya matengenezo ya kawaida kwa ndege hizo zote za Boeing 787-8 (Dreamliner), imepangwa kufanyika kwa pamoja ili kuondoa hatari ya kukosekana kwake kwa muda mrefu ikiwa watapoteza nafasi ya matengenezo waliyopangiwa.

“Huu ni utaratbu wa kawaida kwa Mashirka yote ya ndego duniani. Kama livyo kawaida, utaratibu maalum umeandalwa kwa abiria wote wa safari za Guangzhou, China ill safari zao ziendelea kama kawaida kama walivyofahamishwa hapo awali hadi ndege zitakaporejea,” imesema taarifa hiyo na kuongeza;

“ATCL Itaendelea kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wateja huku kizingatia usalama wa abiria wake ikiwemo kuhakikisha matengenezo yanafanyka kama livyopangwa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!