Monday , 20 May 2024
Home Kitengo Biashara RC Mbeya azindua NMB Onja Unogewe Nyanda za Juu, “ni ubunifu wa kipekee”
Biashara

RC Mbeya azindua NMB Onja Unogewe Nyanda za Juu, “ni ubunifu wa kipekee”

Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amezindua rasmi Kampeni ya Onja Unogewe inayoendeshwa na Benki ya NMB chini ya mwamvuli wa Teleza Kidijitali, inayowezesha malipo kwa njia ya NMB Lipa Mkonono (QR) kwa usalama wa pesa za wafanyabiashara na wanunuzi lengo likiwa kuhamasisha mhamo wa jamii kutoka kwenye matumizi ya pesa taslimu kwenda katika matumizi yasiyo ya pesa taslimu. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera (kushoto) na Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Matawi na Mauzo wa Benki ya NMB, Donatus Richard (kulia)wakipeperusha Bendera kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Onja Unogewe kwa kanda ya nyanda za juu inayolenga kuhamasisha matumizi ya kufanyia malipo kwa njia ya kidigitali kupitia NMB Lipa Mkononi(QR) inayoendeshwa na Benki hiyo katika stendi ya mabasi madogo ya Nane Nane jijini Mbeya.

Akizungumza kuhusu  kampeni ya NMB Onja Unogewe wakati wa uzinduzi katika viwanja vya stendi ya daladala ya Nane Nane jijini Mbeya, Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Matawi ya NMB, Donatus Richard  alisema kuwa, licha ya Onja Unogewe kubeba dhana nzima ya suluhu za kifedha katika manunuzi na malipo, pia kampeni hiyo inawapa fahari wao kama benki katika kujenga mfumo Jumuishi wa masuala ya fedha kupitia mapinduzi ya kidijitali waliyoyafanyia uwekezaji mkubwa.

Donatus alibainisha kwamba, NMB inadhamiria kuhakikisha wafanyabiashara wanapata malipo yao moja kwa moja kwenye akaunti zao tena bila makato yoyote kwao wala wateja – kazi yao ni kuwapa wateja QR kuscan- Hii ni njia rahisi na salama kuhakikisha mahesabu hayapotei na hujihakikishia usalama wa fedha zao.

Moja ya faida anayopata mlipaji kupitia NMB Lipa Mkononi ni kuwa wigo mpana wa kulipia kidijitali na kunufaika na rejesho la hadi asilimia 10 katika malipo atakayofanya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera (kushoto) na Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Matawi na Mauzo wa Benki ya NMB – Donatus Richard (center)wakipeperusha Bendera kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Onja Unogewe kwa kanda ya nyanda za juu inayolenga kuhamasisha matumizi ya kufanyia malipo kwa njia ya kidijitali kupitia NMB Lipa Mkononi(QR) inayoendeshwa na Benki hiyo katika stendi ya mabasi madogo ya nane nane jijini Mbeya. Kulia ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu, Straton Chilongola.

Homera aliipongeza NMB kwa ubunifu na kuwaita ‘nyumba ya ubunifu’. Aidha, aliishukuru NMB kwa kuzindua kampeni hiyo jijini Mbeya, moja ya mikoa ya mpakani (Zambia na Malawi) ambayo inakabiliwa na matukio mengi ya wizi, ujambazi na upotevu wa pesa, huku akiwataka wafanya biashara na wajasiriamali wa Nyanda za Juu kuchangamkia fursa ya kutumia NMB Lipa Mkononi (QR) ili kukabiliana na changamoto hizo katika mauzo na manunuzi yao ya kila siku.

Vile vile, aliwaasa wana Mbeya – hasa watoa huduma za Bajaji, bodaboda, mama lishe, wauza maduka, wafanyabiashara na wajasiriamali, wanapaswa kuwa vinara katika kuchangamkia huduma hii.

Wekeni QR Code hizi madukani na sehemu zenu za biashara, ili kuwawezesha wateja kufanya malipo na kuepukana na mtukio hatarishi kwa fedha zao yanayoikabili jamii, hususani mikoa hio ya mipakani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Sloti ya Wild 81 malipo kwa njia 81 Meridianbet kasino

Spread the love Meridianbet kuna mchezo wa sloti wa kusisimua sanaambao utakufurahisha....

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Biashara

Meridianbet watoa msaada wa chakula Chamazi

Spread the love  JUMAMOSI ya leo Meridianbet wametua pale Chamazi Magengeni kwaajili...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB ‘yafunga ndoa’ na wanawake wanaomiliki shule, vyuo Tanzania

Spread the loveBENKI ya NMB imeingia makubaliano rasmi (MoU) na Chama cha...

error: Content is protected !!