Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wachimbaji wadogo waaswa kuzingatia sheria za madini kupunguza migogoro
Habari Mchanganyiko

Wachimbaji wadogo waaswa kuzingatia sheria za madini kupunguza migogoro

Spread the love

MKURUGENZI wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira, Mhandisi Henry Mditi amewaasa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini kuzingatia sheria, usalama, utunzaji wa mazingira na matumizi salama ya baruti katika uendeshaji wa shughuli za uchimbaji madini ili kupunguza migogoro isiyokuwa na tija migodini. Anaripotit Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Mhandisi Mditi ameyasema hayo leo tarehe 21 Julai 2023 kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba kwenye ufunguzi wa mafunzo ya Usalama, afya, utunzaji wa mazingira na matumizi salama ya baruti kwa wachimbaji wadogo wa madini, yaliyofanyika Wilayani Tarime mkoani Mara.

Mafunzo hayo yameshirikisha pia wakurugenzi, mameneja, watumishi kutoka tume ya madini, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa mkoa wa Mara, viongozi wa wachimbaji wadogo na wachenjuaji wa madini pamoja na wafanyabiashara na wamiliki wa migodi wa eneo la Nyamongo.

Mhandisi Mditi amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuhakikisha kuwa shughuli za uchimbaji na uchenjuaji, na biashara ya madini zinafanyika kwa kuzingatia Usalama, Afya na Utunzaji wa mazingira kwa kufuata Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali iliyowekwa.

“Tunatambua kwamba shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini zina manufaa mbalimbali kwa mchimbaji, wananchi na Taifa kwa ujumla kupitia fursa za ajira, biashara na mapato mbalimbali kwa serikali,” amesema Mhandisi Mditi.

Amesema kuwa mafunzo hayo yameangazia pia utaratibu wa utoaji leseni za uchimbaji, uchenjuaji, biashara ya madini hususan kwenye usimamizi wa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa madini nchini.

” Ni muhimu shughuli hizo kufanyika kwa kuzingatia Usalama, Afya na Utunzaji wa mazingira ili kuzifanya kuwa endelevu kwa vizazi vilivyopo na vijavyo, hivyo mafunzo haya yatiliwe mkazo namna ya kuepuka na ajali migodini, utunzaji wa mazingira, afya na matumizi sahihi ya baruti.” amesema Mhandisi Mditi.

Ameongeza kuwa, “Kupitia mafunzo haya naamini mna wajibu mkubwa wa kuimarisha mfumo wenu wa utendaji kazi kwa kuangalia usalama katika maeneo mnayochimba ili kuhakikisha kuwa taifa halipotezi nguvu kazi ili tuwe na uchimbaji endelevu wa kuimarisha maisha yetu na jamii inayotuzunguka,”

Wachimbaji wa madini 105 kutoka eneo la Nyamongo Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara wameshiriki mafunzo hayo ya siku moja ambapo, wametakiwa kuepuka utoroshaji wa madini kwani kwa kufanya hivyo watasababisha Serikali kukosa mapato na kushindwa kutoa huduma za msingi za kijamii zenye tija ikiwemo elimu bure na afya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!