Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko AG adai ugumu wa maisha chanzo mahabusu kufurahia kukaa rumande
Habari Mchanganyiko

AG adai ugumu wa maisha chanzo mahabusu kufurahia kukaa rumande

Feleshi
Spread the love

 

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, amedai baadhi ya mahabusu ambao makosa yao yanaruhusu kupewa dhamana, wamekuwa wakikataa nafuu hiyo ya kisheria, kwa lengo la kuendelea kukaa mahabusu kutokana na ugumu wa maisha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Feleshi ametoa kauli hiyo leo Alhamisi, katika mkutano wa Tume ya Haki Jinai na wahariri wa vyombo vya habari, Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya swali lililohoji sababu za makosa yasiyokuwa na dhamana kuongezeka, kuibuka.

Dk. Feleshi amesema, kufuatia utafiti uliofanywa kubaini sababu za magereza kujaa mahabusu na watuhumiwa, ilibainika kuwa baadhi ya mahabusu hufurahia kukaa rumande.

“Mwelekeo wa sasa ukiangalia ujazo wa magereza yetu twende na takwimu 2007 magereza yetu kwa siku ilikuwa na wahalifu 47,000 wakafikia mpaka 37,000. Lakini tunapoongea leo tuko na 33,000 au 32000 na wakati huo tuko na 47,000 idadi ya mahabusu ilikuwa 26,000 na wafungwa 21,000 mpaka ilifanyika utafiti ikaulikana magereza mawili kila siku ujazo wake ulikuwa unashangaza. Ilikuwa Tarime na Kahama,” amesema Dk. Feleshi.

Dk. Feleshi amesema “Survey iliyofanyika magereza ya Kusini mojawapo Lindi, tukakuta mahabusu wengi makosa yanadhaminika ila wao wanafurahia kuwa ndani, zikaja sababu za kiuchumi kwamba magereza pamoja na shida iliyopo kuna uhakika wa mlo mmoja, kuangalia TV.”

Kuhusu ongezeko la makosa yasiyokuwa na dhamana, Dk. Feleshi amesema tume imependekeza makosa yasiyokuwa na dhamana yapunguzwe hadi kufikia matano, kutoka takribani 50 idadi ya iliyopo sasa.

“Tume imefanya kazi kubwa ndiyo maana mapendekezo mnayoona mojawapo ni kurejewa upya kwa sheria ya uhujumu uchumi na makosa ya kupanga, kwa nia ya kupunguza makosa ambayo hayadhaminiki,”amesema Dk. Feleshi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!