Saturday , 18 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Jaji Mwangesi: Wanao-park STK baa tupeni taarifa tuwashughulikie
Habari MchanganyikoTangulizi

Jaji Mwangesi: Wanao-park STK baa tupeni taarifa tuwashughulikie

Spread the love

KAMISHNA wa Maadili Jaji Sivangilwa Mwangesi ametoa wito kwa Watanzania kutoa taarifa pindi wanapobaini kiongozi wa umma anatumia vibaya mali za umma kwa masilahi binafsi ikiwamo matumizi ya magari ya serikali katika sehemu zisizofaa kama vile baa. Anaripoti Gabriel Mushi…(endelea.)

Katibu Idara ya Ukuzaji Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. Waziri Kipacha, akitoa mada iliyohusu Ukuzaji wa Maadili katika mkutano huo.

Pia amesema kama zipo taarifa za uhakika kwamba baadhi ya viongozi wa umma wameandika majina ya uongo kuhusu umiliki wa mali zao, wananchi watoe taarifa kwa Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa umma ili wachukuliwe hatua.

Jaji mwangesi ameyasema hayo katika mkutano wa Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa umma na Wahariri wa vyombo vya habari nchini uliofanyika tarehe 17 Juni2023 Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo ulilenga lengo la kujadili mambo mbalimbali yenye kujenga afya katika uwasilishaji wa taarifa kutoka kwenye mamlaka hiyo kwenda kwa jamii.

Alisema kuwa tasnia ya habari ni mhimili muhimu unaofanyakazi ya kupokea taarifa kutoka vyanzo mbalimbali na kuzipitia kisha kuzifikisha kwa wananchi kwa lengo la kuhabarisha umma.

Alisema anaamini kuwa wahariri wakielewa vizuri majukumu yanayotekelezwa na taasisi husika, ni wazi kuwa jamii itafikiwa na taarifa sahihi zilizopitiwa na kuchakatwa kitaalamu.

“Tunaamini kuwa ninyi mkielewa vizuri mtaisadia jamii kuielewa vizuri Mamlaka ya taasisi yetu, na mtaitendea haki taaluma yenu na mtazichakata vizuri habari zozote ambazo zitawafikia katika madawati yenu kuhusiana na viongozi wa umma na ukiukwaji wa mahadili kwa viongozi wa umma. Mtazihoji na kuzidadisi taarifa hizo, kuzipembua na kuziangalia matakwa na mazingatio ya Sheria.

“Katika mkutano wetu huu wa malengo yetu ni kuongeza ushirikiano kati yetu na nyinyi Wahariri wa vyombo habari ili kutoa taarifa sahihi, kubadilishana mawazo ,kupeana ushuri wenye afya ili kujenga kitu kizuri kutoka kwetu kwenda kwa umma. alisema Jaji Mwangesi na kuongeza kuwa;

“Tunaamini kuwa taarifa zetu zikiwa kamilifu, kupitia kwenu, majukumu na mamlaka yetu kwa mujibu wa ibara ya 132 ya mujibu wa Katiba yetu ya Tanzania wa mwaka 77, na Sheria ya Maadili ya viongozi wa umma namba 13 ya mwaka 1995, ambazo ni Sheria tunazozifanyia majukumu yake zitaeleweka vizuri kwa wadau wetu.

“Hivyo ni muhimu kwenu ninyi Wahariri kujua msingi wa mambo muhimu ambayo Taasisi yetu ingependa kuwajulisha viongozi na wananchi kupitia vyombo vya habari” aliongeza Jaji Mwangesi.

Akizungumzia kuharibika kwa Maadili, Jaji Mwangesi alisema sasa hivi suala la Maadili ni kilio kila kona hapa nchini, na kusisitiza kuwa sasa ni jukumu la watu wote kujua namna ya kukabiliana nal tatizo hilo na kulitatua.

Aidha, Katibu Idara ya Ukuzaji Maadili, Waziri Kipacha akitoa mada kuhusu ukuzaji wa maadili, alieleza kuwa lipo tatizo la vijana kuingia kwenye mitandao ya kijamii na kuiga mitindo ya maisha ya kigeni na kusahau mila na desturi za Kitanzania ambazo zinapaswa kuheshimiwa na kulindwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua bima ya afya kwa wakulima

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni...

Habari Mchanganyiko

Makamba awasili China kwa ziara ya kikazi

Spread the loveWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Ethiopia yafungua njia ujenzi wa ubalozi Dodoma

Spread the loveSerikali ya Tanzania imeipongeza Serikali ya Ethiopia kwa kuweka historia...

error: Content is protected !!