Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanavijiji waikumbuka sekondari iliyokosa maabara kwa miaka 17
Habari Mchanganyiko

Wanavijiji waikumbuka sekondari iliyokosa maabara kwa miaka 17

Spread the love

WANAVIJIJI wa Kata ya Bukumi, wilayani Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara, wamejenga maabara tatu za masomo ya sayansi katika Shule yao ya Sekondari Mtiro, ambayo wanafunzi wake wameikosa huduma hiyo kwa miaka 17 tangu ilipoanzishwa 2006. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 11 Machi 2023 na Ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, wanavijiji hao wamepanga kufanya ujenzi  wa maabara hizo katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia tarehe 13 Machi mwaka huu.

“Tarehe 9 Machi 2023, Prof. Muhongo aliendesha harambee shuleni hapo kwa lengo la kupata fedha za ujenzi wa maabara tatu za masomo ya fizikia, kemia na bailojia za Mtiro Sekondari, matokeo yake fedha zilizochangwa taslimu ni Sh. 494,000, ahadi Sh. 4.49 milioni, saruji mifuko 26 na mchanga roli Tano,” imesema taarifa hiyo.

Ofisi hiyo imesema kuwa, Prof. Mujongo ameanza kuchangia ujenzi huo kwa kutoka mifuko 150 ya saruji.

Imesema ujenzi wa maabara hizo unatarajiwa kukamikika Juni, 2023.

Imesema shule ya Sekondari Mtiro Ina wanafunzi 682, ambapo 42 pekee ndiyo wanasoma masomo ya sayansi, huku ikiwa na walimu 17, wanne kati yao ni wa kujitolewa huku 13 wakiwa waajiriwa serikalini.


Kupitia taarifa hiyo, Prof. Muhongo amewataka wadau wengine wa maendeleo kutoa michango yao Kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya elimu jimboni humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

error: Content is protected !!