Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kada NCCR-Mageuzi aliyepotea aokotwa porini akiwa taabani, hajitambua
Habari za Siasa

Kada NCCR-Mageuzi aliyepotea aokotwa porini akiwa taabani, hajitambua

Edward Sembeye, Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma wa NCCR Mageuzi
Spread the love

 

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Jovine Clinton, aliyepotea tangu tarehe 24 Januari 2023, amepatikana akiwa hajitambui katika pori lililoko nje ya Jiji la Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi na Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma ya NCCR-Mageuzi, Edward Simbeye, akizungumza na waandishi wa habari na kusema Jovine ameonekana usiku wa kuamkia tarehe 31 Januari mwaka huu.

Simbeye amedai kuwa Jovine aliokotwa na wananchi akiwa porini hajitambui, ambapo walitoa taarifa Polisi na kwamba hivi sasa anapatiwa matibabu na hali yake kiafya inaendelea kuimarika.

“Leo naomba nitoe taarifa ya awali kwamba Jovine aliokotwa porini, ndani ya msitu mnene na wasamaria wema nje ya Mkoa wa Dar es Salaam akiwa kwenye hali mbaya ya kutojitambua na waliwataarifu Polisi kisha Jeshi la Polisi likawajibika kwa mujibu wa majukumu yao,” amesema Simbeye.

Simbeye amesema NCCR-Mageuzi inalitaka Jeshi la Polisi kuendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini waliohusika na tukio hilo kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria.

Kupatikana kwa Jovine kumekuja ikiwa zimepita siku tatu tangu Jeshi la Polisi lionyeshe kusudio la kuanza kufanya uchunguzi wa kisayansi dhidi ya mawasiliano yake, ili kubaini watu aliowasiliana nao kabla ya kupotea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yatoa kauli wanaolala nje Hospitali ya Muhimbili

Spread the loveSERIKALI imesema inajipanga kushirikiana na sekta binafsi kujenga majengo yatakayosaidia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara yaomba bajeti ya Sh. 67.9 bilioni, wamachinga watengewa bilioni 10

Spread the loveBAJETI ya Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yahamasisha uanzishaji vituo vya kulea watoto wachanga

Spread the loveSERIKALI imewahimiza wananchi kujenga vituo vya kulelea watoto wadogo na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

error: Content is protected !!