Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Sh bilioni 60 kujenga barabara ya lami Mbinga
Habari Mchanganyiko

Sh bilioni 60 kujenga barabara ya lami Mbinga

Spread the love

 

ZAIDI ya Sh bilioni 60 zinatarajiwa kujenga kilometa 35 za lami katika Kijiji cha Amanimakoro hadi Kijiji cha Ruanda – wilayani Mbinga mkoani Ruvuma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ruvuma … (endelea).

Akitoa taarifa ya ujenzi huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Ephatar Mlavi amesema mradi huo unahusisha ujenzi wa barabara ya lami ya Kitai hadi Lituhi yenye urefu wa kilometa 82.

Ameutaja mradi huo unaotekelezwa na Mkandarasi kutoka kampuni ya China Railway Seventh Group ulianza kutekelezwa tarehe 15 Juni, 2022 na unatarajiwa kutekelezwa kwa miezi 18, hadi Desemba 2023.

Amesema mradi huo unahusisha ujenzi wa kilometa 35 za barabara kwa kiwango cha lami, ujenzi wa madaraja manne, ujenzi wa makalaveti makubwa saba na ujenzi wa makalavati madogo 58 na kwamba hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 24 .Tayari serikali imetoa fedha za kujenga kilometa 40 kati ya 82.

“Barabara hii ina umuhimu mkubwa katika usafirishaji wa makaa ya mawe kwa sababu eneo hili lina migodi mingi ya madini hayo hivyo barabara hii itasaidia usafirishaji wa makaa ya mawe Kwenda sehemu mbalimbali nchini ikiwemo bandari ya Mtwara,’’ amesisitiza Mhandisi Mlavi.

Akizungumza baada ya kukagua mradi wa barabara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Laban Thomas amempongeza Mkandarasi kwa kufanya kazi ndani ya mkataba ambapo amesisitiza kazi hiyo ikamilike mapema ili wananchi waanze kunufaika nayo.

Ameitaja barabara ya Kitai-Lituhi kuwa ni miongoni mwa barabara kubwa mkoani Ruvuma yenye urefu wa kilometa 82 ambayo inategemewa na mkoa katika kukuza uchumi na kwamba inaunganisha wilaya za Mbinga na Nyasa, pia inaunganisha Mkoa wa Ruvuma na Njombe kupitia wilaya ya Ludewa.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuchukua uamuzi wa kizalendo wa kutekeleza mradi huo unaoufungua Mkoa wa Ruvuma kupitia barabara ya Kitai-Lituhi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!