Tuesday , 21 May 2024
Home Habari Mchanganyiko TEF yateta na wabunge mabadiliko sheria za habari
Habari Mchanganyiko

TEF yateta na wabunge mabadiliko sheria za habari

Spread the love

 

JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limefika bungeni jijini Dodoma kwa ajili ya kuzungumza na wabunge kuhusu namna ya kufanikisha mchakato wa marekebisho ya sheria za habari nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Leo Jumanne, tarehe 8 Novemba 2022, Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, kwa kushirikiana na wadau wengine, wamefanya mazungumzo na Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa, kuhusu marekebisho hayo.

Akizungumza nje ya viwanja vya Bunge, Silaa ameahidi kushirikiana na wabunge wenzake katika kuhakikisha tasnia ya habari inakuwa na Sheria rafiki na zinazotekelezeka.

“Mimi na wabunge wenzangu tutashirikiana, dunia imebadilika na hatuwezi kubaki hapa tulipo. Nitazungumza na wenzangu na kisha tutaona mamna ya kufanya,” amesema Silaa.

Akizungumza katika mkutano huo, Balile amesema Sheria ya Huduma za Habari ya 2016 imeweka mazingira magumu yanayomdhoofisha mwandishi wa habari kutekeleza majukumu yake.

“Katika safari ya mabadiliko haya, tumeungana na taasisi zote za habari ili kuwa na kauli moja. Tumeunganisha nguvu ili kufikia lengo,” amesema Balile.

Deudatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF)

Mbali na TEF, taasisi nyingine za habari zinazoshiriki katika mchakato huo ni Wadau wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA), Tawi la Tanzania.

James Marenga, Mjumbe wa CoRI kutoka Taasisi ya Vyombo ya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania alimweleza Silaa kwamba, tasnia ya habari haina tofauti na tasnia zingine nchini katika utendaji kazi.

Marenga ambaye ni wakili wa kujitegemea amesema, ikiwa mawakili wanatengeneza taratibu zao na kuzifanya kuwa rejea katika kazi zao, inashindikanaje wanahabari nao wakajiwekea utaratibu wa ‘kujihukumu’ kama ilivyo tasnia nyingine?

‘‘Mimi ni mwanasheria, katika taasisi yetu tulitengeneza codes of conduct wenyewe na hizo ndio zinatuongoza, ni busara na wanahabari wakawa na utaratibu wao kisheria unaosimamiwa na wenyewe katika kuhakikisha maadili ya uandishi wa habari yanafuatwa,’’ amesema.

Jessy Kwayu, Mkurugenzi Mkuu wa Media Brains Inc Ltd amesema, sheria ya habari ya mwaka 2016 ilipitishwa katika mazingira ambayo si rafiki.

‘‘Vipengele 19 vya sheria hiyo vilijaribiwa kwenye sheria za nchi, vikaonekana kutoingia katika mizani ya kisheria,’’ amesema Kwayu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hukumu mahakama kuu yabatilishwa kesi State Oil, Equity Bank Tz

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imebatilisha hukumu iliyotolewa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Geita, Mwanza waongoza kwa mbwa

Spread the loveNaibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yapata idhini kuwa wakala wa madalali wa DSE

Spread the loveBenki ya NMB imepata idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania...

error: Content is protected !!