Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Sita wajeruhiwa majibizano ya risasi na polisi
Habari Mchanganyiko

Sita wajeruhiwa majibizano ya risasi na polisi

Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam
Spread the love

 

KAMANDA wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Jumanne Muliro, amesema watu sita kati ya tisa wanaotuhumiwa kwa ujambazi, wamejeruhiwa na risasi wakati wakijibizana na Polisi walipovamia kiwanda kimoja jijini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kamanda Muliro ametoa taarifa hiyo leo Ijumaa, tarehe 22 Julai 2022, alipotembelea kiwanda hicho kilichopo maeneo ya Keko, Dar es Salaam, baada ya kuvamiwa na watuhumiwa hao usiku wa kuamkia leo.

Amesema majeruhi hao wamefikishwa hospitalini kwa ajili ya matibabu, huku watatu waliobakia wakiendelea kuwa mikononi mwa polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

“Jeshi likapata taarifa kwa hiyo Polisi wakaja haraka eneo la tukio wakalikuta kundi hilo la wahalifu ambao majambazi, wakaanza kuwatihsia na kushambulia mmoja alikuwa na silaha, askari wakajihami kwa silaha baadae wakasalimu amri,” amesema Kamanda Muliro na kuendelea:

“Majambazi wapatao sita walijeruhiwa kwenye miili yao na wamepelekwa haraka hospitali kwa matibabu ili tuweze kupata fursa za kuwahoji kwa kina. Wengine tuko nao na uchunguzi wa tukio unaendelea na mali walizotaka kuiba zaidi ya maboksi 70 zimeokolewa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!