Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bilionea pekee Afrika Mashariki anatoka Tanzania
Habari Mchanganyiko

Bilionea pekee Afrika Mashariki anatoka Tanzania

Spread the love

 

KAMPUNI ya Utafiti ya New World Wealth na Henley, inayosaidia watu wenye thamani ya juu kupata makazi ,uraia kupitia uwekezaji, imeasema kuwa bilionea pekee wa Afrika Mashariki anatoka nchini Tanzania. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa Mashirika ya Kimataifa … (endelea).

Kwamujibu wa ripoti hiyo,iliyotolewa na kampuni hiyo , haikuweza kumtaja jina bilionea huyo ni nani, huku watu wengi zaidi wakiingia kwenye safu ya mamilionea wa dola, hata hivyo ripoti ya utajiri ya Afrika mwaka 2022 inaonesha kuwa Tanzania inawatu 2400 wenye thamani ya zaidi dola za Marekani milioni 1,Nation imeripoti.

Ripoti hiyo, ya utajiri wa Afrika ya mwaka 2022, imetokana na data iliyokusanywa na New World Wealth inayohifadhi data ya Henley au Partners ya watu wenye thamani ya juu, inayojumuisha hasa watu wenye cheo cha Mkurugenzi Mtendaji, mwanzilishi na mshirika.

Hata hivyo ripoti inaonesha kuwa zaidi ya nusu ya mamilionea wa dola (1300) wanaishi katika mji mkuu wa kibiashara wa Dar es salaam, huku jiji hilo likiorodhezwa katika nafasi ya 12 kwa utajiri ,na raia binafsi wakiwa na utajiri wa dola bilioni 24.

Katika utafiti huo unaonesha makadirio makubwa zaidi kulikoripoti nyingine, ikionesha ugumu wa kufuatilia matajiri barani Afrika.

Aidha Afrika Kusini ina idadi kubwa zaidi ya mamilionea wa dola,wakiwa 39,300 ikifuatiwa na Misiri (16,900) ,Nigeria (10,000) kulingana na ripoti ya kwanza ya utajiri ya Henley.

Tanzania ilifanikiwa kushika nafasi ya saba tena kwa kuwa na utajiri wa dola milioni 10 au zaidi.Tanzania ina watu 80 wa aina hiyo , nyuma ya Ghana (120), Morocco (220), Kenya (340), Nigeria (510), Misiri (880) na Afrika Kusini (2,080) .Tanzania ikiorodheshwa kuwa ya sita kwa kuwa na idadi kubwa ya watu ikiwa na utajiri wa angalau dola milioni 100.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atangaza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba

Spread the loveSERIKALI imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu ya...

error: Content is protected !!