Saturday , 18 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wasafirishaji washauriwa kubana matumizi badala ya kupandisha nauli
Habari Mchanganyiko

Wasafirishaji washauriwa kubana matumizi badala ya kupandisha nauli

Spread the love

BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC), limeshauri wadau wa usafirsihaji kuziba mianya ya upotevu wa mapato ili kumudu gharama za uendeshaji, badala ya kupendekeza ongezeko la nauli. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo ulitolewa jana Jumanne, tarehe 13 Aprili 2022, jijini Dar es Salaa na Katibu Mtendaji wa LATRA CCC, Leo Ngowi katika kikao cha wadau cha kujadili maoni ya nauli za mabasi.

“Tujadiliane namna ya kuziba mianya ya upetevu wa mapato kunakofanya Sekta ishindwe kukua. Mfano mabasi kwenda mwendo kasi kunaongeza upotevu wa mafuta kwa zaidi ya asilimia 28.99 na matairi ya gari kuisha kwa zaidi ya asilimia 60,” amesema Ngowi.

Ngowi amewataka wasafirishaji kutotumia wapiga debe kwani huongeza gharama za uzalishaji kwa zaidi ya asilimia 40, badala yake waajiri wafanyakazi ambao watawaongezea faida kwa asilimia 30.

“Hayo yakifanyika ingeleta maana zaidi, kulikoni kuomba nyongeza ambayo haitekelezeki,” amesema Ngowi.

LATRA CCC, limetoa mapendekezo hayo baada ya wadau wa usafirishaji kutoa nauli pendekezwa, wakitaka ziongezeke ili waweze kumudu gharama za uzalishaji zinazotokana na kupanda kwa bei ya mafuta, vifaa vya magari na kushuka kwa thamani ya shilingi.

Miongoni mwa mapendekezo hayo ni, nauli za daladala za mjini zipande kutoka Sh. 500 hadi 1,117 kwa umbali wa kilomita 15. Km 10 (Sh. 400-745). Km 20 (Sh. 600-1,490). Km 25 (Sh. 750-1,862) na Km 30 (Sh. 750-2,235).

Kwa safari za mikoani, wapendekeza zipande kutoka Sh. 53.22 hadi Sh. 86.31 kwa kilomita moja. Ambapo nauli kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, imependekezwa ipande hadi kufikia Sh. 83,861.

Hata hivyo, baraza hilo limepnga mapendekezo hayo, likishauri watoa huduma hizo waelekezwe kutumia nauli zilizohimilivu kwa njia mbalimbali.

“Kwa mikoa ambayo bado nauli zilizoidhinishwa bado hazijaweza kutekelezwa kabisa, basi nauli hizo zishushwe ili kuendena na uwezo wa abiria kulipa. Mikoa hiyo ni kama Bukoba, Kigoma, musoma na maeneo mengine,” amesema Ngowi.

Mapendekezo ya LATRA CCC ya kupinga ongezeko la nauli, yalipingwa na wadau wa usafirishaji.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa LATRA, Gillard Ngewe zoezi la upokeaji maoni ya nauli litafungwa ifikapo tarehe 20 Aprili mwaka huu, ambapo amewataka wadau kutoa maoni kupitia njia ya maandishi na mtandaoni.

Ngewe amesema, zoezi hilo likifungwa, LATRA itatangaza bei mpya za nauli nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua bima ya afya kwa wakulima

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni...

Habari Mchanganyiko

Makamba awasili China kwa ziara ya kikazi

Spread the loveWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Ethiopia yafungua njia ujenzi wa ubalozi Dodoma

Spread the loveSerikali ya Tanzania imeipongeza Serikali ya Ethiopia kwa kuweka historia...

error: Content is protected !!