Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kupanda kwa bei ya nauli kwaibua mvutano, wamiliki watishia kusitisha huduma
Habari Mchanganyiko

Kupanda kwa bei ya nauli kwaibua mvutano, wamiliki watishia kusitisha huduma

Spread the love

MVUTANO umeibuka katika kikao cha wadau cha kujadili bei mpya za nauli kilichoitishwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), baada ya Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri la mamlaka hiyo, kupendekeza mapendekezo ya wadau upandishaji bei yasikubaliwe kutokana na sababu mbalimbali. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Mvutano huo umeibuka leo Jumatano, tarehe 13 Aprili 2022, jijini Dar es Salaam, baada ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri la mamlaka hiyo (LATRA-CCC), Leo Ngowi, kushauri nauli za mabasi yaendayo mikoani zisipandishwe.

Badala yake vitumike viwango vya nauli vilivyopangwa 2013, kwa sababu wahusika hawajafikia viwango hivyo.

“Nauli ya Mwanza ni Sh. 61,400, lakini nauli inayotozwa 4,5000 mpaka 50,000, kuna tofauti ya Sh. 6,400 ambayo msafirishaji hajafikia viwango. Kigoma nauli 78,400, nauli inayotozwa ni kati ya 50,000 mpaka 60,000 ikiwa tofauti ya 18,400. Kwa hali iliyopo sasa pamoja na kampuni bado hawajaanza kutoza nauli zilizioanishwa na mamlaka mpaka leo hi,” amesema Ngowi.

Ngowi amesema “maombi kwa mamlaka tumeleta matatu, kwa za isipokee maombi haya badala yake watoa huduma waelekezwe kutumia nauli zilizohimili ambazo hazinatumiwa.Kwa mikoa nauli zilizoidhinishwa bado haijzajaongezeka, zishushwe kuendana na nauli zilizopita kama Kigoma, Bukoba na hili ni ombi letu kwa malamka .

Kwa upande wa nauli za daladala, Ngowi ameshauri pendekezo la mapendekezo yaliyotolewa na Umoja wa Usafirishaji Abiria Mkoa wa Dar es Dalaam (UWADAR), ya ongezeko la nauli la Sh. 400 akitaka yapitiwe upya kwa kuwa vigezo vilivyotumika kuipanga kutokuwa na uhalisia.

“Baraza limeazimia mamlaka isipokee maombi (ongezeko la Sh. 400 nauli ya daladala Dar es Salaam), mpaka yafanyiwe maboresho, wayarudishe tena ili tuangalie gharama zinazotozwa. Nauli za sasa ziendelee kutumika,” amesema Ngowi.

Mapendekezo hayo yaliibua mvutano kutokana kwa wadau ambayo wameyaoinga wakidai hayalengi kutatua changamoto iliyopo.

Kutokana na mvutano huo kuwa mkali, Mwenyekiti wa kikao hicho, Alhaji Juma Fimbo, aliwataka wadau kuwa watulivu kwa kuwa kikao hicho kimeitishwa kujadili mapendekezo na sio cha kutoa maamuzi.

“Ondoeni dhana kwamba mamlaka iko kuwakomoa au CCC iko kuwakomoa, haoana. Lengo tufikie uamuzi wa nauli ambazo zitakidhi vigezo,” amesema Alhaji Fimbo.

Wadau hao walipinga mapendekezo hayo wakitaka bei za nauli zipande ili kuendana na kupanda kwa gharama za uendeshaji ikiwemo bei ya mafuta.

Akizungumza katika kikao hicho, Nuru Mohammed Ally, amesema kama mapendekezo yao hayatafanyiwa kazi watasitisha kutoa huduma.

“Gharama zimepanda mara mbili anasema watu wasisikilizwe, huyu wasipoangalia biashara inafungwa. Wasipoangalia biashara inafungwa sababu tulikuwa tunasukumana,” amesema Nuru.

Awali, Mwakilishi wa kampuni ya usafirishaji Happy Nation, Ally Siddy Urasa, alipendekeza nauli ya Dar es Salaam-Mwanza, ipande hadi Sh. 8,3861.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

error: Content is protected !!