Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ayapa majeshi changamoto mpya
Habari za Siasa

Rais Samia ayapa majeshi changamoto mpya

Kamishna wa Magereza, Meja Jenerali, Suleiman Mzee
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema anataka mwelekeo mpya wa majeshi kuachana na uzalishaji mali na kuwekeza nguvu zaidi katika majukumu yao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo ameyasema leo Ijumaa tarehe 25 Machi 2022 jijini Dodoma mara baada ya kuzingdua miradi mbalimbali ya jeshi la Magereza.

Mkuu huyo wa nchi na amiri jeshi mkuu, amesema umefika wakati sasa kila jeshi lianzishe mashirika ya uchumi na kuajiri wataalam ambao si askari ili wawafanyie kazi na kuongeza uzalishaji zaidi.

Amesema kufanya hivyo si jambo jipya kwani nchi zingine tayari wanafanya hivyo na kuyataka majeshi kwenda kujifunza kwao.

“Suala la uzalishaji linayahusu majeshi yetu yote na nimeshaona kial jeshi linajitahidi kwa namna moja au nyingine kufanya shughuli za uzalishaji kuongeza kipato ili jeshi liendelee na shughuli zake.”

Amesema mweleko yanayokwenda nao majeshi yanaelekea kufanya kazi ndogo zinazowahusu huku “msukumo mkubwa” ukienda kwenye uzalishaji mali, “na tukiendelea hivi tutakuta tunazalisha mali kweli kwenye jeshi, tunapata fedha za kujiendesha lakini zile nyanja za medani hatuzipi uzito wake.”

Amesema kutokana na hali hiyo mwaka ujao wa fedha Serikai imeamua kuongeza fedha ndani ya vikosi vya majeshi yake ili wajielekeze zaidi kwenye kazi zao zinazowahusu kuliko uzalishaji mali.

“Suala la uzalishaji mali halipukiki lakini hapa ndipo napotaka niungane na Mh. Waziri kwamba tuna rasilimali nyingi lakini hatuzitumii kikamilifu,” amesema na kuongeza “hiyo ni kwasabbu hatuna uwezo wakuzitumia.”

“Sasa kama tutajipanga vizuri kila jeshi likawa na shirika lake la uchumi Jeshi kwa mfano wana JKT lakini wakawana na chombo kingine cha kuangalia uchumi wa jeshi lao, labda polisi hivyohivyo NA magereza na mengine.

Rais Samia Suluhu Hassan

“Mashirika haya yakapewa wataalamu wanaoweza kuyaendesha kibiashara wakasimamia biashara za majeshi yao wakawa ndiyo trust wakaingia mikataba na sekta binafsi wakaweza kuendesha biashara kwa niaba ya majeshi yao.

“Na zoezi hili hatulianzi sisi huko ulimwenguni yanafanyika na yapo na majeshi yanapata fedha zao kupitia mtindo kama huo.

Niwatake majeshi yetu kwenda kujifunza kwa wenzetu duniani wanajifanya vipi mpaka majeshi yanazalisha miradi mikubwa bila kuacha kazi zao za msingi,” amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yatoa kauli wanaolala nje Hospitali ya Muhimbili

Spread the loveSERIKALI imesema inajipanga kushirikiana na sekta binafsi kujenga majengo yatakayosaidia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara yaomba bajeti ya Sh. 67.9 bilioni, wamachinga watengewa bilioni 10

Spread the loveBAJETI ya Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yahamasisha uanzishaji vituo vya kulea watoto wachanga

Spread the loveSERIKALI imewahimiza wananchi kujenga vituo vya kulelea watoto wadogo na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

error: Content is protected !!