Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanawake wawaongoza wanaume Chou cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Z’bar
Habari Mchanganyiko

Wanawake wawaongoza wanaume Chou cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Z’bar

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere nchini Tanzania, Stephen Wasira amesema, shabaha ya chuo hicho ni kutoa elimu endelevu kwa wote ikiwa ni pamoja na wanawake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Wassira ambaye pia ni waziri mstaafu amesema hayo jana Jumatatu, tarehe 29 Novemba 2021, katika mahafali ya sita ya Kampasi ya Karume Visiwani Zanzibar.

Amesema hayao baada ya takwimu kuonesha, kati ya wahitimu 1,242 aliowatunuku wa ngazi mbalimbali za astashahada, stashahada na shahada wanawake ni 749 sawa na asilimia 60 ya wahitimu wote na wanaume ni 493 sawa na asilimia 40.

Aidha, Wasira ameipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano ambao chuo kimekuwa kikipata hivyo kusaidia kufikia malengo ambayo imejiwekea.

Awali, Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Prof. Shadrack Mwakalila amesema idadi ya wahitimu wanawake katika chuo hicho imezidi kuongezeka mwaka hadi mwaka.

Amesema chuo kimeanza ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi 1,536 ambapo bweni la wavulana litakuwa na uwezo wa kubeba wanafunzi 768 na la wasichana 768 na ujenzi utakamilika tarehe 18 Desemba 2022.

Prof. Mwakalila amesema, katika Kampasi ya Karume, Mshauri elekezi tayari ameshakamilisha michoro kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za wafanyakazi 30. Aidha, mchakato wa kumpata mkandarasi wa kujenga nyumba hizo unaendelea.

Pia, Prof. Mwakalila akitoa taarifa ya maendeleo ya chuo amesema, mshauri elekezi ameshakamilisha michoro ya ujenzi wa Madarasa na Mabweni kwa ajili ya Tawi la Pemba ambalo lilifunguliwa rasmi Machi 2020 ikiwa ni sehemu ya jitihada za chuo kusogeza huduma karibu na wahitaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atangaza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba

Spread the loveSERIKALI imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu ya...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza namna Nathwani alivyomjeruhi jirani yake

Spread the loveMSIMAMIZI wa Msikiti wa Wahindi Lohana aitwae, Ankit Dawda (32)...

error: Content is protected !!