Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ashikiliwa Takukuru kutorejesha milioni 44 kwa miaka kumi za Saccos
Habari za Siasa

Ashikiliwa Takukuru kutorejesha milioni 44 kwa miaka kumi za Saccos

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Manyara, inamshikilia mkazi wa Mjini Babati, Yuda Sendeu akidaiwa kuzuia Sh. 44.7 milioni fedha za chama cha kuweka na kukopa cha Babati Saccos. Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara … (endelea).

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Manyara, Holle Joseph Makungu akizungumza mjini Babati leo Jumamosi tarehe 8 Agosti 2020 amesema, Sendeu alichukua mkopo wa Sh.35 milioni na kutakiwa kurejesha Sh.44.7 milioni.

Makungu amesema, Sendeu alichukua mkopo huo mwaka 2010 na alitakiwa kurudisha mkopo huo baada ya miezi 24 pamoja na riba.

Amesema uchunguzi unaonyesha Sendeu alifanya makubaliano ya kihalifu na baadhi ya wanachama wa Babati Saccos waliochukua fedha katika Saccos hiyo bila kurejesha.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Manyara, Holle Joseph Makungu

Amesema walifanya hivyo ili haki za wanachama waaminifu wa Saccos hiyo ziweze kupotea.

“Hadi wanachama waaminifu wa Saccos hiyo wanafikisha malalamiko ya dhuluma hiyo Takukuru, Sendeu bila kustahili amekaa na fedha hizo kwa miaka 10,” amesema Makungu.

Ametoa rai kwa wanachama wa Babati Saccos wanaofahamu kuwa wamechukua fedha za Saccos hiyo na muda wa kurejesha umepita wafike kwa hiyari kwenye ofisi za Takukuru.

Amesema wanatakiwa wafike kwenye ofisi hizo tarehe 10 Agosti 2020 ili wapewe hesabu zao na kuzirejesha na kwa wale watakaokaidi hatua kali dhidi yao zitachukuliwa kuanzia 12 Agosti 12 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!