Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Naibu Waziri aimwagia sifa CCBRT
Afya

Naibu Waziri aimwagia sifa CCBRT

Spread the love

NAIBU Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel ameipongeza hospitali ya CCBRT kwa utendaji kazi mzuri licha ya kuwepo changamoto zinawaikabili hospitali hiyo. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam …. (endelea).

Waziri Mollel ameyasema hayo alipotembelea hospitali hiyo leo tarehe 1 Julai 2020 iliyoko Msasani jijini Dar es Salaam katika ziara isiyo rasmi na kukutana na kusalimiana na uongozi wa hospitali hiyo.

Amesema kuwa ameamua kuitembelea hospitali hiyo kwakuwa imekuwa ikiendelea kushirikiana na Serikali kwa muda mrefu kutoa huduma bora za  afya kwa watanzania wenye mahitaji. 

“Nawafahamu CCBRT na kazi mnazozifanya kwa muda mrefu sasa, nawapongeza kwa kazi nzuri, kama Serikali tunatambua mchango wa hospitali hii katika kuwahudumia watanzania, leo nimefika kusalimia kidogo lakini naahidi kuja rasmi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja ili tuweze kupata wasaa wa kujadilina kwa kina juu ya kazi zenu,” amesema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali hiyo, Brenda Msangi amemshukuru Dk. Mollel kwa kufika CCBRT, na kumueleza ambavyo taasisi yake inanufaika na ubia kati yake na serikali tangu kuanza kwake hadi hapa ilipofikia.

“Kwa niaba ya wafanyakazi wenzangu wa CCBRT napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Serikali yetu kupitia Wizara ya afya tumekuwa tukipata msaada na ushirikiano mkubwa  kutoka serikalini kwa hili, nasema asante sana na naomba utufikishie salam zetu kwa dada yangu Ummy Mwalimu na watendaji wake wote,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

error: Content is protected !!