September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tanzania yafika uchumi wa kati

Spread the love

BENKI ya Dunia (WB) imeitangaza Tanzania kuingia katika nchi za uchumi wa kipato cha kati. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hatua hiyo imefikiwa miaka mitano kabla ya lengo la Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inayobainisha kufikia mwaka huo, Tanzania itafikia uchumi wa kati.

Leo Jumatano tarehe 1 Julai 2020, Rais wa Tanzania, John Magufuli ametumia akaunti yake ya Twitter kutoa pongeza kwa Watanzania kwa kufikia hatua hiyo.

Rais John Magufuli

Rais Magufuli amesema, “Benki ya Dunia leo tarehe 01 Julai, 2020 imeitangaza Tanzania kuingia uchumi wa kati.”

“Nawapongeza Watanzania wenzangu kwa mafanikio haya. Huu ni ushindi mkubwa na kazi kubwa tumeifanya, tulipanga kuingia uchumi wa kati ifikapo 2025 lakini tumefanikiwa 2020. Mungi Ibariki Tanzania,” amesema Rais Magufuli.

error: Content is protected !!