Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Michezo Yanga sasa rasmi bila Manji
Michezo

Yanga sasa rasmi bila Manji

Yusuf Manji
Spread the love

WANACHAMA na mashabiki wa Yanga sasa wanapaswa kujiandaa kisaikolojia kuishi maisha bila Yusuf Manji baada ya jina la mwenyekiti huyo kutokuwapo miongoni mwa wagombea 27 waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa klabu hiyo utakaofanyika Janauri 13, 2019. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Tofauti na ilivyotarajiwa Manji hajachukua wala kuchukuliwa fomu kama ambavyo kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilitaka Yanga wafanye endapo watahitaji kumrejesha mwenyekiti huyo, badala yake wanachama wanne wamejitokeza kuwania nafasi hiyo.

Mwanasheria wa TFF, Herman Kidifu aliwataja wagombea waliojitosa kuwania nafasi ya Mwenyekiti ni Dk Jonas Tiboroha, Yono Kevela, Mbaraka Igangula na Erick Ninga.

Wanaowania nafasi ya makamu mwenyekiti ni Titus Osoro, Salum Magege Chota na Kevela wakati wajumbe ni Hamad Ally Islamu, Benjamin Jackson Mwakasonda, Sylvester Haule, Salim Seif, Musa Katabaro, Shftu Amri na Said Baraka.

Wengine ni Pindu Luhoyo, Dominick Francis, Seko Jihadhari, Ally Omary Msigwa, Arafat Ally Haji, Geofrey Boniphace Mwita, Frank Kalokola, Ramadhan Said, Leonard Marango, Bernard Faustin Mabula, Christopha Kashiririka, Athanas Peter Kazige na Faustin Peter Bisangwa.

Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wakili Ally Mchungahela alisema mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu umefungwa rasmi na keshokutwa Ijumaa utafanyika mchujo kwa wagombea wote.

“Uchaguzi uko palepale kwa wagombea waliochukua fomu, baada ya mchujo wa Ijumaa kutakuwa na usaili na baadaye wagombea wataingia kwenye kampeni kuelekea katika uchaguzi,” alisema Mchungahela.

Mchungahela alitoa onyo kwa mtu yeyote atakayejaribu kujipenyeza kuvuruga mchakato wa uchaguzi kwa kuanzisha vurugu, kuwa vyombo vya dola vitafanya kazi yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!